SERIKALI imeamua kuunda kikosikazi kitakachohusisha Idara ya Usalama wa Taifa, Polisi wa Kimataifa (Interpol) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya kuanza uchunguzi kuhusu Watanzania wanaotuhumiwa kuficha kiasi cha Sh314 bilioni nchini Uswisi.
Hatua
hiyo ya uchunguzi inatokana na Bunge kutoa maazimio ya kuitaka
Serikali kufuatilia sakata hilo katika kikao chake kilichopita mjini
Dodoma na kutoa majibu katika kikao cha Bunge cha Aprili mwakani.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema, “Tuhuma hizo siyo jambo dogo na Serikali haiwezi kuzipuuza, sasa tunachukua hatua madhubuti.”
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema, “Tuhuma hizo siyo jambo dogo na Serikali haiwezi kuzipuuza, sasa tunachukua hatua madhubuti.”
Jaji Werema alisema kuwa Serikali imeshapiga hatua katika kufanya uchunguzi huo.
“Tumepiga hatua katika suala hili, ila ukianza kusema sana utakuwa unaharibu. Tumeamua kuwa na kikosi maalumu cha upelelezi kitakachoshirikisha Idara ya Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Wizara ya Fedha na wachunguzi binafsi wakiwamo Polisi wa Kimataifa (Interpol) pamoja na Benki ya Dunia (WB).

“Serikali
inaweza kuwashirikisha watu wengine kama Benki ya Dunia (WB) na Polisi
wa Kimataifa (Interpol) kwa ajili ya kusaidia uchunguzi huo.”
Aliongeza
kuwa katika timu hiyo, wameamua kumshirikisha Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutaka
ukweli wa sakata hilo.
“Tumeamua kulifuatilia jambo hili, kama tutafanikiwa litakuwa jambo jema. Kama hatutafanikiwa tutakuwa tumejaribu,” alisema.
Hata hivyo, Werema alisema kuwa, bado hawajamwita Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa ajili ya ushauriano zaidi.
Hata hivyo, Werema alisema kuwa, bado hawajamwita Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa ajili ya ushauriano zaidi.
“Unajua
kuwa mwanasheria mkuu siyo kujua kila kitu, Zitto pia anaweza akawa na
mbinu, ambazo zitasaidia katika jambo hili,” alisema Werema.
Uchunguzi
Hivi karibuni akiwa jijini Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika alisema kuwa Serikali ya Uswisi imeitaka Tanzania kuwasilisha kwake majina ya watu wanaotuhumiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini humo, kama sharti la kusaidia uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.

Hata
hivyo, kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na gazeti moja la
Kiingereza nchini, maofisa wa Uswisi walitaka ushahidi zaidi wa majina
kama sharti la kutoa ushirikiano katika uchunguzi huo.
Kwa
mujibu wa habari hizo, maofisa hao waliwataka wenzao wa Tanzania
kupeleka majina ya wahusika, pia kutoa ushahidi usio shaka unaoonyesha
nani alimpa nani rushwa, kuonyesha mazingira ya rushwa yaliyosababisha
kupatikana kwa fedha hizo.
Maofisa hao pia walitaka Serikali ya Tanzania kuonyesha jinsi fedha hizo zilivyohamishwa hadi kwenye benki zao.
Maofisa hao pia walitaka Serikali ya Tanzania kuonyesha jinsi fedha hizo zilivyohamishwa hadi kwenye benki zao.
Kauli ya Zitto
Akizungumzia masharti hayo, Zitto alisema uchunguzi utakaofanywa utafuata mfumo wa uchunguzi binafsi na kubainisha kuwa, kufuata mfumo wa kiserikali kunaweza kuwa na vikwazo vingi.
“Sisi
hatufuati mfumo wa kiserikali, mfumo wa kiserikali ndiyo una masharti
hayo. Sisi tunafuata mfumo wa uchunguzi binafsi,” alisema Zitto.
Akizungumzia masharti hayo, Zitto alisema uchunguzi utakaofanywa utafuata mfumo wa uchunguzi binafsi na kubainisha kuwa, kufuata mfumo wa kiserikali kunaweza kuwa na vikwazo vingi.
No comments:
Post a Comment