Mtoa
habari alisema tukio hilo lilitokea maeneo ya Iliboru mida ya saa tano ya asubuhi ya leo kijana huyo anaishi na ndugu
zake katika nyumba ya kupanga kama
kawaida yake alimuita mtoto huyo ndani ya chumba chake ndipo alipomfanyia kitendo
cha kinyama mtoto huyo mwenye miaka 2
anayeitwa Schola Yakobo.
Tukio
la ubakaji lilishutukiwa na wapangaji wa jirani ambapo walivamia chumba hicho
na kuanza kumpa kichapo cha mbwa mwizi na baada ya dakika kadhaa walimpeleka
kituo kikuu cha polisi,Jijini Arusha.
Mtoto wa miaka 2,Schola Yakoba |
Akiendelea
kuelezea shuhuda wa tukio la ubakaji wa mtoto wa miaka 2 ,Mtuhumiwa alipohojiwa
na polisi alisema ni kweli alimbaka mtoto huyo!!! na kusema kuwa ni shetani
kampitia alikuwa hajitambui.
Shuhuda
mwingine ambaye pia ni mpangaji katika nyumba moja na mama wa mtoto(Jina
kapuni) aliyebaka alisema kuwa Abdul ni kawaida yake ,Kwani si mara ya kwanza
kufanya tukio la namna hiyo bado ana kesi ya ubakaji mahakamani jijini Arusha.
Chanzo
hiki kilibahatika kufanya mahojiano na mama mzazi wa mtoto huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Mariam
Millah akiwa wodi namba 9 ya wazazi hospitali ya mkoa ya Mlima meru(Mt.meru) mida ya saa nane mchana
wa leo alisema ni kweli mtoto wake kabakwa na kijana huyo,Abdul ambaye anaishi jirani nae.
Alikuwa
akitokwa na machozi wakati wa mahojiano huku akiwa karibu na mwanae kwenye
kitanda katika wodi hiyo.
Mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Millah akiwa wodi namba 9 ya wazazi hospitali ya mkoa ya Mlima meru(Mt.meru) |
Chanzo
chetu cha habari kilibahatika kuona hali ya mtoto huyo,yupo katika hali mbaya
sana akisubiria matibabu ndani ya wodi ya wazazi ya Mt.Meru.
Mpaka
chanzo chetu cha habari hii kinaondoka eneo la hospitali
ya mlima meru Schola Yakobo mtoto
aliyebakwa alikuwa bado ajapatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment