EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, December 22, 2012

Yaliyojiri baina ya Lulu na Kanumba yaanikwa.


Msanii wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu' (katikati) akiingia mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana Ijumaa


UHUSIANO wa kimapenzi baina ya msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' anayedaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, umewekwa wazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya msanii huyo kukiri kuwa alikuwa na uhusiano na Kanumba.

Upande wa serikali jana Jumatatu ulisoma maelezo ya mashahidi tisa wanaotarajia kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo pamoja na maelezo ya Lulu aliyoyatoa Kituo cha Polisi Oysterbay, ambayo ni moja ya vielelezo vitakavyowasilishwa mahakamani wakati kesi itakapoanza kusikilizwa rasmi.

Akisoma maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando, Wakili wa serikali, Shadrack Kimaro, alidai kuwa Lulu alitoa maelezo hayo Aprili 7 mwaka huu katika kituo cha polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam mbele ya askari wa kituo hicho, Sajenti Renatus.

Alidai kuwa Lulu alizaliwa mwaka 1994 na kwamba ana elimu ya Kidato cha Nne aliyoihitimu katika Shule ya Sekondari ya Midway, baada ya hapo aliendelea na shughuli za sanaa ambazo alizianza tangu mwaka 2000.
Alidai kuwa Lulu alifahamiana na Kanumba kwa muda wa miaka 10 wakifanya kazi za sanaa na Januari mwaka huu ndipo walipoanza rasmi uhusiano ya kimapenzi.

Alidai kuwa katika uhusiano huo hawakuwahi kuishi pamoja isipokuwa alikuwa akienda kwa Kanumba anapojisikia na mara kadhaa aliwahi kulala huko.

Wakili huyo alidai kuwa katika kipindi cha miezi minne ya uhusiano wao, walikuwa wakigombana mara chache lakini sababu kubwa ilikuwa ni wivu wa mapenzi kwa sababu wote walikuwa hawaaminiani.

Pia Wakili huyo alidai kuwa Aprili 5, mwaka huu Kanumba na Lulu walitumiana ujumbe mfupi wa simu.

Alidai kuwa jioni ya siku hiyo Lulu alimpigia simu Kanumba na baada ya muda mfupi alikwenda nyumbani kwake Sinza Vatican.

Alidai kuwa alipofika kwa Kanumba, alimkuta akiwa chumbani kwake akinywa pombe ambayo ilikuwa imechanganywa na soda na ghafla simu yake iliita na alipotoka nje kutaka kwenda kuisikiliza Kanumba alimfukuza hadi barabarani.

Alidai kuwa baada ya kumfukuza alimkamata na kuanza kumpiga vibao na mateke huku akilalamika kwamba anamdharau na alimpeleka hadi chumbani ambapo alichukua panga lililokuwa chini ya kitanda na kuanza kumpiga kwa ubapa.

Alidai kuwa baada ya kumpiga kwa ubapa ghafla alitupa panga chini huku akiwa amesimama alianza kupumua kwa taabu na baada ya muda mfupi aliyumba na kujigonga ukutani na kuanguka chini.

Alidai baada ya kuanguka, Lulu alikimbia na kwenda kujifungia chooni kwa hofu na baada ya muda alitoka na maji na kwenda kummwagia Kanumba lakini hakuamka.
Siyo mimi niliyemuua nilimkuta amekunywa pombe na alikasirika sana kupita kiasi...siwezi kumsukuma ila yeye anaweza kunifanya atakavyo,alidai Lulu.

Alidai kuwa baada ya kuona hali hiyo alishikwa na hofu na kuamua kukimbia kwenye ufukwe wa Coco Beach. Alidai kuwa akiwa huko alipewa taarifa kuwa Kanumba amefariki na ndipo alipompigia simu rafiki yake ili aende kumsaidia kuendesha gari waelekee kwenye msiba.

Uchunguzi wa awali wa polisi ulionyesha kuwa hakukuwa na jeraha lolote kuanzia kichwani hadi mwilini kwa Kanumba.

Inadaiwa kuwa uchunguzi wa kifo hicho ulifanywa na jopo la madaktari watatu na daktari mmoja wa familia kutoka hospitali ya Amana ambapo ulibaini kuwa ubongo wa Kanumba ulikuwa umevimba na damu imevilia.

Baada ya uchunguzi huo sampuli kadhaa kama kucha za mikono yote miwili, majimaji ya machoni, ini, figo, damu vilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya kusomwa maelezo hayo Hakimu Mmbando alimuhoji Lulu kama ana lolote la kuongea na baada ya kujadiliana na Wakili wake, Lulu alijibu kuwa hana cha kuongea.
Kesi yenu kwa hapa Kisutu imefikia mwisho kwa hiyo jalada litapelekwa Mahakama Kuu tayari kwa kuanza kusikilizwa...utaendelea kukaa mahabusu hadi utakapoletewa wito wa kufika Mahakama Kuu,alisema Hakimu Mmbando na kuahirisha kesi hiyo.CHANZO CHA HABRI NI MWANASPORT.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate