MKAZI wa Kijiji cha Nyankorongo wilayani Chato, mkoani Geita,
Lameck Maraba (29), amejiua kwa kujikata koromeo baada ya kuhisi ana
ugonjwa wa ukimwi muda mfupi baada ya kushauriwa na daktari kupima afya
yake.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi baada ya kijana huyo
kushitushwa na ushauri wa daktari aliyemtaka kupima afya yake ili
kubaini magonjwa yanayomkabili.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilayani hapa, Pius Buchukundi alisema
mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo Januari 17, akisumbuliwa na homa
ya matumbo, malaria na upungufu wa damu ambapo kutokana na hali hiyo
alishauriwa kupima VVU.
Aliongeza kuwa kutokana na ushauri huo, aliingiwa hofu na kuamua kujikata koromeo na kusababisha kifo chake.
Pamoja na hilo, mganga huyo ametoa ushauri kwa wagonjwa wanaokwenda
kutibiwa, wafuate ushauri unaotolewa na wauguzi ili kuepusha vifo
visivyo vya lazima.
Jeshi la Polisi wilayani hapa limethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha kusikitisha.
No comments:
Post a Comment