Askari watano
wanaotuhumiwa kuhusika na upotevu wa Sh. milioni 150 zilizoporwa katika
tukio la ujambazi eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam wanaendelea na
kazi kama kawaida huku Jeshi la Polisi likipata kigugumizi kwa kushindwa
kuweka wazi majina yao.
Taarifa ambazo NIPASHE imezipata kutoka kituo cha polisi Kati (Central) jijini hapa, zimeeleza kuwa siku mbili baada ya siri kuvuja kwamba askari waligawana fedha hizo zilizodondoshwa na majambazi waliitwa na kuhojiwa kituoni hapo.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuhojiwa baadhi ya askari hao walikutwa na kiasi fulani cha fedha ambazo inasadikiwa kuwa ni sehemu ya Sh. milioni 150 zilizopotea katika mazingira ya kutatanisha wakati wa tukio la ujambazi.
Hata hivyo, tangu askari hao waitwe na kuhojiwa, inaeleza kuwa kila siku wamekuwa wakienda Kituo Kikuu cha Polisi na kusaini kitabu cha mahudhurio kwamba wapo kazini.
Hali hiyo imewashangaza askari wengine ambao wamekuwa wakihoji inakuwaje wenzao waliotuhumiwa kuiba fedha hizo wanaendelea na kazi wakati wengine wakifanya makosa kama hayo husimamishwa kazi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alipoulizwa na NIPASHE jana kuhusu kinachoendelea kuhusu askari hao na kwanini majina yao hayawekwi wazi kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine.
Kamanda Kova alisema suala la askari hao hapendi kuliongelea kupitia simu na kuahidi kuwa atalitolea maelezo kwa kuitisha mkutano na waandishi, hata hivyo hakueleza lini atafanya mkutano huo.

Suala la askari hao nitaitisha ‘press conference’, siku hizi sipendi kuliongelea jambo lolote kwa simu nimegundua kuna baadhi ya waandishi wanapenda kunilisha maneno ambayo sikuyasema.
Hata hivyo, wakati Kamanda Kova akikwepa kuweka wazi majina ya askari hao, NIPASHE imefanikiwa kuyapata.
Ingawa kwa sasa bado (NIPASHE) tunasitiri majina yao kwa kuwa hatujafakiniwa kuwapata ili wazungumzie tuhuma zinazowahusu, vyeo vyao, mmoja ni Sajini Taji (SSGT) na wanne ni wenye vyeo vya Koplo. Soma zaidi habari hii kwenye gazeti la NIPASHE

No comments:
Post a Comment