MMOJA
kati ya waimbaji bora wa muziki wa dansi waliowahi kutokea hapa nchini,
Cosmas Thobias Chidumule, amefiwa na mwanae wa kike Damaris Chidumule
“Dotto” (35).
Binti huyo wa Chidumule alifariki juzi (Jumatatu) baada ya kuugua ugonjwa wa malaria na anatarajiwa kuzikwa leo.
Marehemu Damaris Chidumule “Dotto”
Kwa
mujibu wa mtoto mwingine wa Chidumule, Omoka Chidumule ambaye ni mdogo
wa marehemu, aliiambia Saluti5 jana jioni kuwa dada yake atazikwa leo
(Jumanne) mchana katika makaburi ya Kinondoni.
Cosmas Thobia Chidumule
Msiba upo Kinondoni Mahamkamani nyumbani Chidumule.
Cosmas
Chidumule ambaye kwasasa anejitosa kwenye muziki wa injili, bado
hajafutika kwenye ramani ya muziki wa dansi hususan kutokana na tungo
zake zilizotukuka kama vile “Barua kutoka kwa mama Part 1 na part 2)”, “Neema”,
“Kata ya maji ukweni” na nyingine nyingi kupitia bendi za DDC Mlimani
Park “Sikinde” na Orchestra Safari Sound “Ndekule”.
Via saluti5.
No comments:
Post a Comment