WADAU WACHANGAMKIA FOMU ZA UONGOZI TFF
WADAU wa michezo wamejitokeza kuchukua
fomu za kugombea nafasi mbali mbali za uongozi wa shirikisho la soka
nchini ( TFF) utaotarajia kufanyika Februali 24 mwaka huu.
Makamu wa Pili wa (TFF), Ramadhan Nassib, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya makamu wa Rais.
Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura, alisema kuwa jana ikiwa ndio siku ya kwanza kwa uchukuaji wa fomu hizo, wadau 19 wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Wambura alisema kuwa licha ya Nassib, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Wallace Karia nae amechukua fomu kuwania nafasi hiyo.
Alisema kwa upande wa waliochukua fomu za ujumbe ni Shaffih Dauda, Athuman Kambi, Hussein Mwamba, Stewart Masima, Yusuph Kitumbo na Mugisha Galibona.
Wengine ni Vedastus Lufano, Twahili Njoki, Charles Mugondo, Elley Mbise, Farid Nahdi, Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja, Epaphra Swai, Khalid Abdallah, James Mhagama na Selemani Bandiho.
Wambura alisema mchakato wa uchukua fomu utaendelea hadi Januari 18, mwaka huu, saa 10 jioni.
Alisema nafasi zitakazowaniwa ni Rais wa shirikisho hilo, Makamu wa Rais na wajumbe 13 wa kamati ya utendaji ya TFF.
Wambura alisema gharama ya fomu kwa nafasi ya rais wa TFF ni shilingi 500,000, makamu wa rais wa TFF ni shilingi 300,000 na wajumbe ni 200,000.
Alisema kamati ya uchaguzi ya TFF, itapitia fomu za waombaji uongozi kuanzia Januari 19 hadi 21, ambapo watatangaza majina ya waombaji uongozi waliopitishwa.
No comments:
Post a Comment