Sakata la mchezaji wa kimataifa wa
Uganda anayeichezea klabu bingwa ya Tanzania Bara Simba SC, Emmanuel
Okwi kwenda kujiunga na kambi ya Simba iliyopo nchini Oman limefikia
mwisho.
Kwa taarifa za ndani kutoka ndani ya klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo imefikia maamuzi ya kumuuza mshambuliaji huyo kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya uhamisho hapa nchini ya $300,000.
Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Simba Mh. Aden Rage kwa sasa yupo nchini Tunisia akisimamia taratibu zote za uuzwaji wa Okwi ambaye alisaini mkataba mpya wa kuitumikia Simba hivi karibuni.
"Ni
kweli Mwenyekiti yupo Tunisia akishughulikia uuzwaji wa Okwi kwa klabu
ya Etoile du Sahel. Ada ya uhamisho ni dola laki tatu na muda mchache
ujao dili litakamilika na Okwi atapewa ruhusa ya kuzungumza maslahi
binafsi na klabu yake mpya." - kilisema chanzo cha habari kutoka ndani
ya Simba. Kwa taarifa za ndani kutoka ndani ya klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo imefikia maamuzi ya kumuuza mshambuliaji huyo kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya uhamisho hapa nchini ya $300,000.
Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Simba Mh. Aden Rage kwa sasa yupo nchini Tunisia akisimamia taratibu zote za uuzwaji wa Okwi ambaye alisaini mkataba mpya wa kuitumikia Simba hivi karibuni.
Etoile du Sahel ni klabu mojawapo yenye mafanikio makubwa barani Afrika, ikiwa inashikilia rekodi ya kuwa klabu pekee barani afrika kushinda kila kombe linaloandaliwa na CAF.
Kwa taarifa zaidi kuhusu ukamilikaji wa dili hili endelea kutembelea tovuti hii.
No comments:
Post a Comment