YACHUKUE
mapenzi halafu itazame timu ya mpira wa miguu, kikapu na hata pete
(netiboli) inavyocheza. Utaona kwamba ni lazima kupeana pasi mpaka mpira
unapofikia mfungaji. Hakuna mwenye uwezo wa kutoka na mpira golini
kwake, akawapita wapinzani 10 na kufunga.
Mpira
ni pasi, yaani kushirikiana kutafuta ushindi. Haitakiwi kutegeana.
Jinsi unavyoona mpira unavyochezwa, ndivyo na uhusiano wa kimapenzi
unavyojengwa. Wewe na mwenzi wako ni timu moja, sasa mnachezaje kutafuta
ushindi?
Je, anapokuwa na mpira, nawe unajipanga vizuri ili akupe pasi halafu umrudishie afunge au kazi yako ni wewe kumtazama anavyokatiza na kumshangilia? Anapokabwa na maadui, unakwenda kumsaidia au yako yanabaki macho tu, yaani akidhibitiwa ubaki unasonya, akishinda mshangilie pamoja?
Akikupa mpira kwenye sehemu nzuri, unafunga goli au utangoja kumrudishia kwa sababu hutaki lawama baada ya kukosa goli? Mtu anayefanya hivi, huyo si mtu sahihi kwenye timu. Ni mtegeaji, kwa maana hiyo kama wewe unakuwa na sifa hii kwenye uhusiano, huhitajiki kabisa.

Uhusiano wa kimapenzi hujengwa na watu wawili wanaoamua
kucheza kama mbio za vijiti. Mmoja anakimbia umbali wake halafu
anamkabidhi mwenzake ili amalizie. Hupaswi kukimbia peke yako ili
mwenzako abaki mtazamaji au mshangiliaji, vilevile hutakiwi kuwa
mtegeaji. Nendeni pamoja.
Hata kama mwenzi wako ameonesha kuwa na kasi kubwa kwenye utafutaji na anafanikiwa, hebu hakikisha nawe unakuwa sehemu ya hayo mafanikio. Wanasema nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa, yupo mwanamke jasiri na imara.
Kadhalika, nyuma ya mwanamke mwenye mafanikio, yupo mwanaume shupavu, muungwana, mwana demokrasia. Wanaume wa mifumo dume, mara nyingi huwa hawataki wanawake wao wapambane na kufanikiwa. Eti badala ya kufurahia mafanikio ya mwenzi wake, huona wivu.
Nakubaliana na ukweli kwamba wanawake wengi waliofanikiwa,
hugeuka mwiba wa kuumiza kwa wenzi wao. Hii inasababishwa na udhaifu wa
kisaiokolojia ambao upo ndani ya vichwa vya wanawake kuwa wao hupaswa
kuhudumiwa zaidi. Hata kama mwenzi wako ameonesha kuwa na kasi kubwa kwenye utafutaji na anafanikiwa, hebu hakikisha nawe unakuwa sehemu ya hayo mafanikio. Wanasema nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa, yupo mwanamke jasiri na imara.
Kadhalika, nyuma ya mwanamke mwenye mafanikio, yupo mwanaume shupavu, muungwana, mwana demokrasia. Wanaume wa mifumo dume, mara nyingi huwa hawataki wanawake wao wapambane na kufanikiwa. Eti badala ya kufurahia mafanikio ya mwenzi wake, huona wivu.
Nakubali kuwa kuna wanaume wavivu, eti nao hutaka kuhudumiwa na wapenzi wao. Muda wote wanashinda wamelala halafu ikifika usiku, wanataka wabadili viwanja vya starehe wakajirushe. Naunga mkono watu wa aina hiyo kuadhibiwa. Wavivu hawatakiwi.
Hata hivyo,
sijawahi kuona mwanaume anamuacha mke kwa madai kwamba hachangii
chochote kwenye pato la familia. Hii inatokana na ukweli kwamba
imeshajengeka hivyo na ni ngumu kutengua kuwa mwanaume ndiye mtoa
huduma, hata kama mke atakuwa anashinda nyumbani na kubadili saluni kwa
kujipamba.
Wapo ambao hawataki wapenzi wao watoke kwenda kutafuta. Anataka akatafute peke yake halafu arudishe nyumbani akatumie na mama watoto wake. Ukweli ni kuwa aina hii ya watu, ni wale wanaosumbuliwa na wivu wa kupindukia. Anaogopa mpenzi wake akifanya kazi, ataibiwa.

Hata wanawake, wengine hawataki kuwa mbali sana na wenzi wao. Anachotaka
ni muda mzuri wa kupumzika na mpenzi wake japo kipato kitakuwa kidogo.
Anamaanisha wakiingiza kidogo tu kinatosha. Mwenzi wake akiwa mbali ni
mgogoro. Atauliza: “Kazi sawa lakini na mimi nikae na nani muda huu?”
Siku zote nasimamia mapenzi na maisha. Inatakiwa wanaopendana wawe mstari wa mbele kupigania maendeleo yao. Hivyo basi, sikubaliani na mtindo wa kujifungia muda mwingi, badala ya kushirikiana katika kuongeza kipato. Inawezekana leo kinawatosha kwa sababu mpo wawili, mtoto akija je?

Ni lazima watu wafanye kazi kwa bidii. Kila mmoja aone anao
wajibu wa kupambana kuongeza kipato kwa mwenzake. Hata kama huna kazi,
je, unafanya nini kuhakikisha mpenzi wako hatetereki wakati
anakuhudumia? Pengine mawazo yako yanajenga sana.
Usiwe mtu wa kukaa, kusubiri ufanyiwe kila kitu. Mtoto wa kike kazi yake kupiga mizinga. Anatendewa hili kesho anaomba lingine bila kujiuliza yeye anatoa nini kumwezesha mpenzi wake. Mtindo wa kungoja kupewa, hatari yake ni kubwa. Wapenzi wengi wameachana baada ya mmoja kuhisi anaelemewa na mzigo.

KWA wanandoa ni afadhali lakini wapenzi ambao hawajaoana athari yake
huwa ni kubwa sana. Inawezekana akajitahidi kutoa lakini utoaji
unaendana na uwezo. Akihisi ni mzigo ataona afadhali na mapenzi yafe.
Zingatia, kutaka kupewa bila kujiuliza wewe unachangia nini ni mapenzi
ya kizamani. Tafadhali sana, usiwe wa kizamani.
Wakati unajiongeza kwamba unashindwa kubadilika kutokana na wakati, tambua kuwa mtindo wako wa kimaisha unakufanya uonekane mzigo mzito kwa mwenzio. Tambua kuwa mzigo huwa haukumbatiwi, kwa kawaida aliyeubeba hutamani kuutua. Akifanikiwa kuutua, hupumua.
Kwa mantiki hiyo, tabia zako zinaweza kumfanya mpenzi wako ajisikie amani siku akiachana na wewe. Na kwa kukuongezea ni kwamba hakuna kitu kibaya kama mwenzi wako aone nafuu ya kuwa bila wewe, hapo ni lazima ujue kuna matatizo ambayo yapo ndani yako.

NI ASILI MBAYA
Mtu ambaye anataka apewe zaidi, mara nyingi anakuwa na kasoro za kimaumbile. Huyo anakuwa ni mbinafsi kwa sababu chake kinakuwa ni cha kwake peke yake lakini cha mwenzake anataka kukiwekea sauti. Mara nyingi wanakuwa hatari kwa sababu husumbuliwa na nongwa.
Atataka apewe hata kikiwa hakipo. Anapokosa huhisi kanyimwa. Mtu wa aina hiyo siyo tu kwamba hafai kwenye mapenzi bali hata kwenye maisha ya kawaida kijamii. Hachangii wenzake wanapokuwa wanahitaji michango lakini yeye asipochangiwa ni nongwa.
Mapenzi ni jinsi ambavyo moyo unaridhika, inapotokea mtu anaanza kujiuliza maswali mengi kuhusu mpenzi wake, maana yake anakuwa anamtilia wasiwasi. Pale wasiwasi unapoendelea ndivyo na kiwango cha mapenzi hupungua. Hali hiyo inapozidi, mapenzi hufa kabisa.
Hujawahi kuona watu wanaishi, kila mtu anajua ni wapenzi lakini ndani yao ni kama hakuna kupendana. Yaani wanaishi kwa mazoea tu! Moja ya sababu za wapenzi kufikia hatua hiyo ni mmoja kumuona mwenzake ni mzigo mzito kuubeba.
Tabia hiyo ni sumu hatari kwa maana wapo walioshindwa kupata wenzi wa maisha yao, kwani kila mmoja alimkimbia. Maisha magumu lakini wewe hutaki kutambua hilo, badala yake unataka mahitaji lukuki. Unapaswa kujiuliza wewe umefanya nini?
Angalau basi, kama wewe ni wa kupewa, ufanye juu chini kuhakikisha unapunguza matumizi. Ila wewe ndiye mkali wa kuongeza mahitaji. Ni rahisi kuachwa kwa sababu mtoaji atakapoanza kujiuliza, mwisho wa maswali yake atapata jibu kuwa wewe ni mnyonyaji.

CHUKUA MUONGOZO HUU
Hebu ishi kwa mtindo wa kula na kipofu. Yeye anakupa, sasa kazi kwako kuhakikisha unampa faraja na amani. Ana fedha, wewe huna, kwa hiyo mahitaji yako yanamtegemea yeye, jitahidi kujikomboa ili nawe uwe unaingiza kipato cha kukutosheleza na wakati unapigania hilo, hakikisha unakuwa faraja yake.
Inakuwaje uombe vocha ya simu lakini akikupa, simu unawapigia wengine. Akupigie yeye tu. Nani kakudanganya kwamba yeye ni zezeta wa kiwango hicho? Atakuacha katika kipindi ambacho wewe umetunga kiburi kwenye kichwa chako kuwa hawezi kufurukuta mbele yako.
Ni utani kuamini kuwa hana ujanja mbele yako. Asilimia kubwa walioweka kiburi cha namna hiyo, mwisho walipata shida baada ya kuachwa. Mapenzi hujengwa na vimelea vyake ambavyo ni upendo, heshima na utu. Kama kimoja kati ya hivyo hakuna, hayatafika popote. Yatakufa!

Atakupenda kama nawe unampenda.
Anapokuwa anaonesha upendo wa hali ya juu kwako lakini yeye humpi,
itafika kipindi atakuona hufai. Ataanza kupunguza, mwisho atachoka
kabisa. Hii ndiyo sababu ya kukwambia ‘unapopewa, jiulize nawe unatoa
nini’. Zingatia kuwa mapenzi ya upande mmoja ni ya kizamani.
Usitarajie heshima kutoka kwa mwenzi wako ikiwa wewe humheshimu. Namna unavyo mtendea ndivyo unavyokaribisha uhusika wake kwako.

Itaendelea wiki ijayo.
Via Global Publishers
No comments:
Post a Comment