HATIMA ya maofisa watatu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),
wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi,
itajulikana mwishoni mwa mwezi huu, baada ya ripoti ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kubaini madudu ndani ya shirika
hilo.
Mwenyekiti wa
Bodi ya Tanesco, Jenerali Mstaafu Robert Mboma, alisema kazi ya
kuwachunguza maofisa hao iliyokuwa ikifanywa, imekamilika na wamepewa
ripoti inayoonyesha kuwa kuna kasoro hasa katika ununuzi usiyofuata
taratibu na ubadilishaji wa fedha za kigeni (Dola). Alisema kwa sasa
bodi ipo katika mchakato wa kuunda jopo la watu sita litakalowaita
maofisa hao na kuwahoji na kwamba kila mmoja atatakiwa kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Maofisa hao ambao wanasubiri uamuzi wa Bodi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Ununuzi Harun Mattambo.
Maofisa hao ambao wanasubiri uamuzi wa Bodi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Ununuzi Harun Mattambo.
“Awali CAG alileta taarifa ambayo tuliikataa na kumtaka airekebishe. Hii ya mara ya pili tuliikubali na tumeielewa, kikubwa alichogundua ni ununuzi yusiyofuata taratibu na suala la kubadilishwa kwa Dola za Marekani katika benki ambazo Shirika halina akaunti,” alisema Mboma na kuongeza;
“Benki ambayo Shirika halina akaunti na ambayo wangeweza kubalishia fedha hizo ni Benki Kuu (BOT) pekee, lakini haikufanyika hivyo jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu.”
Alisema baada ya jopo kumaliza kuwahoji watuhumiwa hao, litawasilisha mapendekezo kwa bodi ambayo itatoa uamuzi wake.
Maofisa hao walisimamishwa kazi Julai 14 mwaka jana sambamba na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando, ambaye baadaye alifukuzwa kazi.
Baada ya kusimamishwa kazi kwa maofisa hao, Bodi ya Tanesco ilimpa kazi CAG kuchunguza tuhuma zilizokuwa zinawakabili pamoja na Mhando. Hata hivyo, Bodi ilisema kwa kosa alilolifanya Mhando hawezi kushtakiwa mahakamani kwa sababu makosa aliyoyafanya ya kuingia kwenye mikataba yenye mgongano wa kimaslahi ni kosa la kiuadilifu.
No comments:
Post a Comment