MASTAA wawili wamuziki, Beyoncé Knowles na mumewe Jay-Z wameteketeza kiasi cha dola 80,000 karibu pauni 50,000 (zaidi ya milioni 120 za kitanzania) kumnunulia mwanasesere binti yao kwaajili ya sherehe yake ya kwanza ya kuzaliwa.
Doli huyo maalumu kwa binti yao Blue Ivy amepambwa pia kwa vito 160 pamoja na dhahabu nyeupe.
Blue Ivy mtoto Jay Z na Beyonce
Waimbaji
hao wenye utajiri mkubwa,pia waliandaa pati ya aina yake kwaajili ya
watu wa karibu wa familia na jamaa wengine kwaajili ya kupamba siku hiyo
maalum kwa bintiyao.
Birthday
hiyo iliyofanyika New York ilijumuisha pia pauni 60,000 zilizotumika
kwaajili ya maua meupe na pinki ya waridi kwaajili ya mapambo na keki
iliyo gharimu pauni 1,500.
Pauni
nyingine 20,000 ilitumika kwaajili ya vifaa vingine na midoli kwaajili
ya wageni watoto wa Blue Ivy, zikiwemo seti za vito mbalimbali na nyumba
za kuchezea.
Wageni watu wazima walipewa vifurushi vilivyo wekwa tiketi za tamasha na kalamu maalum za dhahabu.
Beyonce
ambaye ni staa wa kundi la Destiny’s Child akiwa na miaka 31, narapa
Jay-Z mwenye miaka 43, walitangazwa kuwa seti ya mastaa wanandoa
wanaolipwa zaidi duniani mwaka jana baada ya kukusanya pauni milioni 48
katika kipindi cha miezi 12.
Mastaa
hao walitumia wiki kadhaa kupanga sherehe kwaajili ya binti yao, ambaye
alifikisha umri wa mwaka mmoja, Jumatatu ya wiki iliyopita – Januari 7.
“Wanafanya kazi kwa bidii kwaajili ya fedha na jambo la kwanza wanataka kuzitumia kwaajili ya mtoto wao wa kike.
“Ni
vigumu kufikiria ni vipi wanaweza kufanya zaidi ya hivi mwaka ujao — au
miaka yake 16 itakuwaje,”kilisema chanzo cha karibu na wenza hao.
Via saluti5
No comments:
Post a Comment