EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, January 17, 2013

Kamati ya Bunge yaagiza CAG aikague TTB kuhusu ufisadi wa milioni 590/-

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) imebaini ufisadi wa zaidi ya Sh milioni 590 zilizotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Hatua ya kubainika kwa ufisadi huo, hasa wa matumizi yasiyoeleweka ya fedha hizo, iliifanya POAC kuagiza kwa kauli moja kuhakikisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wsa Hesabu za Serikali (CAG) anaifanyia TTB ukaguzi maalumu.

Katika taarifa za hesabu za mwaka wa fedha wa 2010/2011 iliyowasilishwa mbele ya POAC, ilionekana kuwa kuna fedha za bajeti zilizobaki, huku TTB ikishindwa kuziwasilisha Hazina kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Kamati hiyo pia ilihoji sababu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kupeleka bajeti iliyobaki TTB na kutoa agizo fedha hizo zilipwe kwa watu ambao waliwataka wao bila kutaja sababu za watu hao kulipwa fedha hio badala ya kuzipeleka Hazina, hali iliyoonyesha utata juu ya matumizi ya fedha hizo.

Viongozi wa Bodi hiyo walikuwa katika wakati mgumu baada ya kuulizwa sababu iliyowafanya kuwapelekea fedha na kumpa mtu mmoja kuwalipa watu na si Wizara kuchukua jukumu la kuzipeleka Hazina.

Akihoji kwa kutaka kupata ufafanuzi zaidi, Mwenyekiti wa Muda wa Kamati hiyo, Kangi Lugola, alisema zaidi ya Sh milioni 590 ni fedha za bajeti ambazo zilibaki mwaka wa fedha wa 2010/2011 na hazina maelezo zimepelekwa TTB na kulipwa watu kwa shughuli gani badala ya kupelekwa Hazina.

“Kila mwaka inatengwa bajeti kwa ajili ya shughuli ya maonyesho na bajeti inayobaki inatakiwa ipelekwe Hazina, sasa katika eneo hili hatuwezi kuendelea na hesabu zingine hadi tupate maelezo ya kina juu ya matumizi halali ya hizo fedha,” alisema Lugola.

Akitoa ufanunuzi, Mwenyekiti wa TTB, Charles Sanga, alisema Wizara ndio inayoandaa bajeti na wao wamekuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana nao, hivyo mfumo wa Serikali na mashirika ni tofauti, hivyo fedha zinapotolewa zinakuwa na barua na si mkataba.

Naye, Mkurugenzi wa Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Ibrahimu Mussa, alisema wanapopeleka fedha katika maonyesho huwa wana kamati ya pamoja, hivyo kosa lilifanyika kwa TTB na fedha zake zinaendeshwa kwa ruzuku.

Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema haiwezekani mtumishi mmoja wa wizara kuchukua fedha na kwenda kufanya malipo.
via gazeti la MTANZANIA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate