KAMA
kuna watu wanaotakiwa kujua thamani yao na kuitumia kwa faida basi ni
wasanii wa filamu, lakini hali haipo hivyo mwaka 2012 na 2013 umekuwa ni
mwaka wa matukio hususan misiba japo kulikuwa na furaha pia, misiba
ndio iliyotufanya tujue kama wasanii ni matajiri wasio na kitu mkononi.
Msiba
wa marehemu Kanumba ndio uliotufungua na kuamini thamani ya wasanii ni
kubwa lakini haikuwa rahisi kuwezesha mazishi hadi pale ilipoundwa
kamati kwa ajili ya kuchangishana pesa za rambirambi kutoka kwa wadau
mbalimbali na si wasanii wenye, vyombo vya habari vilishika nafasi kwa
kuhakikisha michango inapatikana na mazishi yakafanyika.
Jambo
ambalo ni agharabu kutokea kwa mazishi yoyote katika misiba lilitokea
kila kiongozi awe wa siasa Serikali alihakikisha anafika Sinza Vatican
kwa ajili ya kuhudhuria msiba huo bila kadi ya mwaliko wala nini, kamati
zilikusanya mamilioni ya fedha na mazishi yakafanyika lakini siku ya
siku shutuma zikaja kama kuna watu walijinufaisha na mikwanja ya
marehemu.
Hali
ya kukabana kwa ajili ya wasanii wazikwe imeendelea japo kwa marehemu
Sharo Milionea hakuwa hivyo sijui ilikuwaja lakini hivi karibuni baada
ya rafiki kipenzi cha wapenda filamu Sajuki kufariki bakuli liliendelea
hadi kuna wakati watu waliokuja kuhani msiba walikuwa na hofu kama
wangebanwa kutoa michango ili kupata zaidi ya milioni nane.
Swali ambalo wengi wanajiuliza pamoja na thamani ya wasanii hawa kwani haiendani na maisha yao halisi? Inasemekana
kuwa wasanii hawa hawalipwi malipo stahili lakini jambo baya kuliko
yote ni pale chama cha hakimiliki nja hakishiriki kugeuka kuwa wakala wa
maharamia kwa kuwakandamiza wasanii kwa kuuza haki zao na kubaki kuwa
watu wa mizinga.
Ni maneno yanayouma lakini ukweli ni kwamba tatizo nambari moja wasanii wenyewe hawajijui nini wanahitaji
wapi na kwa wakati gani? Wasanii badala ya kuungana na kutafuta maslahi
ya pamoja badala yake imekuwa ni vita ya kimaslahi wanapokutana kwa
wasambazaji kila mtu akitaka kuwa ni bora kuliko mwingine jambo
linalowapa nafasi wasambazaji kuendelea kuwanyonya.
Serikali
kupitia mamlaka ya mapato imesema inarasimisha filamu na muziki na
tayari tunaona matangazo katika vyombo vya habari ikiwa kama sekta
rasmi, lakini wasanii wanalalamika kuwa hoja kwao si kurasimisha bali
wanataka haki zao zilindwe kwa sababu hawana imani na taasisi kama
Cosota baada ya kuwa ajenti wa wale wanaowadhulumu haki zao, kwa kifupi
ni tatizo ni mikataba na si kingine.
No comments:
Post a Comment