Vinara wa ligi kuu ya England, Manchester United imeambulia pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Tottenham.
Mshambuliaji Robin Van Persie aliiwezesha timu
yake ya Manchester United kuongoza kipindi cha kwanza baada ya kufunga
bao katika dakika ya 25.
Van Persie alipata goli hilo akiunganisha krosi ya Tom Cleverly.
Man United wakiamini kuwa tayari wamepata
ushindi katika mechi hiyo, walijikuta wakigawa pointi baada ya Clint
Dempsey kufunga katika dakika za majeruhi na kuamsha shangwe kwa
mashabiki wa Tottenham katika uwanja wao wa White Hart Lane.
Matokeo hayo bado yanaiacha Manchester United
kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 56, huku ikifuatiwa na Manchester
City yenye pointi 51.
Tottenham iko katika nafasi ya nne ikiwa na
pointi 41, pointi nne nyuma ya Chelsea yenye pointi 45, ikikakalia
nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England.
Timu zote hizo nne zimecheza mechi 23 kila moja.
No comments:
Post a Comment