EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, January 19, 2013

Meya Bukoba Dk. Anatory Amani (CCM) akimbia kikao

MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatory Amani (CCM) amejiweka katika wakati mgumu wa kung’olewa wiki ijayo baada ya kukimbia kikao cha madiwani wa chama hicho kilichokuwa kimjadili.

Katika kikao hicho kilichotawaliwa na vurugu za kurushiana viti baina ya pande zinazopingana, Amani alitumia janja ya kuumwa na hivyo akaondoka kikaoni baada ya katibu wa kikao hicho na msaidizi wake nao kuondoka kwa staili hiyo.
Meya Amani anatuhumiwa na baadhi ya madiwani wa manispaa hiyo kuwa, ametumia vibaya madaraka yake, akijihusisha na vitendo vya ubadhirifu, na hivyo kikao hicho cha madiwani wa CCM kilikuwa kijadili na kupata muafaka wa ama ang’oke mwenyewe au asubiri kupigiwa kura Januari 22.

Tayari madiwani nane wa chama hicho akiwemo Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki na wengine wawili wa upinzani wametia saini hati ya kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo, aitishe kikao cha dharura ili kumng’oa meya huyo.
Habari za ndani kutoka kwenye kikao hicho cha kamati ya uongozi wa madiwani, zilisema kuwa mvutano ulianza mapema kwa wajumbe kupinga Amani asiongoze kikao hicho kwa vile ni mtuhumiwa.

Hata hivyo, vuta ni kuvute hiyo iliendelea na hivyo Amani akaongoza kikao hicho, lakini akalalamikiwa kwa kuwapendelea wale wanaomuunga mkono hatua iliyomkasirisha Diwani wa Kata ya Nyanga, Deusidedit Mutakyahwa kunyanyua kiti na kumpiga Diwani wa Kata ya Kahoro, Chief Karumuna, aliyekuwa akichangia na kumtetea meya huyo.

“Baada ya vurugu hizo Amani alimshawishi Mutakyahwa aende polisi, lakini wajumbe wakawasuluhisha kwa madai kuwa ni ugomvi wa makundi yao. Na kikao kilipoonekana kumbana meya, ghafla katibu aliomba udhuru wa kuondoka,” alisema mtoa taarifa.
Katibu huyo ambaye ni diwani wa viti maalum, Ashura Hassan alidai mtoto wake anaumwa na hivyo kukasimu madaraka yake kwa msaidizi wake, Diwani wa Kata ya Nshambya, Hilde Blandus, ambaye pia baada ya kupokea kiti aliomba udhuru akidai mama yake ni mgonjwa. 

“Huu ulikuwa ni ujanja uliopangwa mapema kwani hata Meya Amani muda mfupi alidai kuwa amechoka kutokana na sindano za Quinine hivyo asingeweza kuendelea na kikao, akaondoka bila kukifunga,” alisema.
Kwamba Amani aligoma pia kuwapa wajumbe muhtasari wa kikao cha kamati ya siasa ya wilaya kilichopita akidai kuwa katibu aliondoka nao.
Kufuatia hali hiyo, madiwani waliazimia kusonga mbele na hoja yao katika kikao cha ‘full council’ cha wiki ijayo Januari 22, kitakachoamua kwa kura za madiwani wa vyama vyote kama ang’oke au la.

Taarifa za ndani zinadai kuwa, rushwa imeanza kutembezwa kwa baadhi ya madiwani wa vyama vyote ili kuwarubuni wasipige kura ya kumng’oa meya.
Baadhi ya vigogo wa serikali akiwemo mkuu wa wilaya na mkoa, mwenyekiti na katibu wa chama tawala Mkoa wa Kagera, wamekuwa wakifanya kila juhudi kumnusuru Amani asing’olewe.

Halmashauri hiyo ina madiwani 24; watatu wa CUF, wanne wa CHADEMA na 17 wa CCM. Ili kupitisha uamuzi huo wa kumuondoa meya, ni lazima robo tatu ya madiwani, yaani 16, wapige kura ya kuunga mkono hoja hiyo.
Miongoni mwa vigogo waliosaini hati ya kutaka kuitishwa kikao cha kumng’oa meya huyo ni Naibu wake, Alexander Ngalinda (Diwani wa Kata ya Buhende) na Yusuf Ngaiza (Kashai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Bukoba.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate