TASNIA ya sanaa ni nyanja ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa
ikitawaliwa na amani, huku watu wake wakionekana kuwa na furaha na
kufanya kazi zao kwa kujitolea zaidi licha ya mapato kiduchu kutokana na
kazi zao.
Hata hivyo, kwa takribani mwezi mmoja sasa imekuwa
ni mshikemshike. Amani inaanza kutoweka taratibu, huku Wizara ya Habari
Vijana, Utamaduni na Michezo ikiwa imelifumbia macho suala hili.
Katika majadala huo kuna baadhi ya wasanii
walieleza wazi tatizo hilo, huku wakiwatuhumu baadhi ya viongozi wakubwa
wanaoaminiwa kuwalinda wasanii, ambao nao pia walikuwapo katika kikao
kile.
Jacob Steven JB, Vicent Kigosi Ray na Bahati Bukuku ni baadhi ya wasanii ambao walitoa dukuduku zao mbele ya Naibu Waziri, huku wakimtuhumu Mtendaji wa Cosota Yustus Mkinga aliyekuwapo katika kikao kile na Makatibu wa Wizara na watendaji wengine wakishuhudia hilo.
Wasanii walitoa ya moyoni, ambayo hata hivyo wizara iliahidi kuyashughulikia lakini hakuna hatua iliyochukuliwa licha ya mhusika kukaa kimya.
Wasanii waliamini kuwa wangesikilizwa na mhusika
angewekwa chini na kuulizwa. Januari ilifika na wasanii wakaendelea na
kazi zao kama kawaida.
Wasanii hawakupata majibu kwa muda mwafaka.
Waliandika barua nyingine, lakini bila kupata majibu hivyo wakaamua
kuitisha kikao chao na waandishi wa habari Januari 20 na kuelezea
dukuduku lao kabla ya kuamua kuandamana nchi nzima. Ingawa inafahamika
kuwa wasanii wa filamu na michezo ya kuigiza wameshauriwa kuzisoma
nyaraka mbalimbali za
Bodi ya Filamu ili wajue sheria na kanuni zinazohusu tasnia hiyo, wao wamedai kuwa zimekuwa zikiwanyonya sana.
Bodi ya Filamu ili wajue sheria na kanuni zinazohusu tasnia hiyo, wao wamedai kuwa zimekuwa zikiwanyonya sana.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce
Fissoo aliwahi kutoa ufafanuzi juu ya Sheria namba 4 ya Utengenezaji wa
Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976.
Fissoo alisema sheria hiyo ndiyo inayoendelea
kutumika hadi sasa na kukanusha taarifa zilizosambazwa na baadhi ya
vyombo vya habari kuhusu uwepo wa matumizi ya sheria mpya.
Alisema hakuna sheria mpya ya Filamu na Michezo ya Kuigiza iliyotungwa, Sheria inayoendelea kutumika ni ile ya mwaka 1976, bali kilichofanyika ni utekelezaji wa kanuni za sheria ya filamu na michezo ya kuigiza, ambapo mchakato wake ulianza mwaka 2011.
Aliwahi pia kuzungumzia kuhusu malalamiko ya
baadhi ya wasanii kushindwa kuhimili kulipa ada ya Sh500,000, Fissoo
alisema kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinampa mamlaka waziri mwenye
dhamana husika kutoa msamaha wa malipo kwa msanii mchanga atakayeshindwa
kulipa kiasi hicho cha fedha.
Kwani? Ada wanayolipa wasanii ya Sh500,000 ipo toka siku za
nyuma, ambapo Sheria Namba 4 ya Filamu na Michezo ya Kuigiza inampa
mamlaka waziri husika kutoa msamaha kwa msanii mchanga atakayeshindwa
kulipa ada hiyo. Kwamba, msamaha utatolewa pale msanii atakapotoa
taarifa kwa waziri na mara baada ya kujiridhisha, ndipo atapitisha
msamaha na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali.
Hata hivyo, wasanii wao wanadai hawana imani na
watendaji wakuu kutoka Cosota na Bodi ya Filamu Tanzania, hivyo
kumemtaka Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua hatua dhidi ya viongozi
hao.
Lalamiko lao msingi wake ni kwamba, hawawezi
kwenda katika urasimishaji wakitumia kanuni ambazo baadhi ya vipengele
vyake vipo kwa lengo la kumkandamiza msanii na mwandaaji wa filamu.
Kwa kawaida ukaguzi wa ‘script’ unagharimu 60,000
kwa saa mpaka 100,000 na itategemea filamu husika itakaguliwa kwa saa
ngapi, huku ukitakiwa kulipia kibali cha kuandaa filamu 500,000
kinachodumu kwa miezi mitatu.
Kwa sasa ni kama vile wezi wa kazi za wasanii
hawaiogopi Cosota kabisa na hawa ndiyo marafiki wakubwa na sekta hiyo
iliyoundwa na Serikali kuliko wasanii ambao ndiyo chanzo cha uwapo wake.
Mfano ulio wazi ni kwamba, Chama cha Waigizaji
Mkoa wa Mwanza kilikamata wezi wa kazi za wasanii cha ajabu tena kwa
jeuri mwizi huyo huku akitamba alimpigia simu Yustus Mkinga kumtaarifu
kukamatwa kwake, na baada ya hapo akaachiwa polisi.
Suala hili linajenga hisia gani kwa wasanii?
Unadhani wana imani na Cosota na kama Cosota iliundwa kwa nia ya
kumsaidia msanii, ni kwa nini kina Bahati Bukuku wanafukuzwa wakifika
Cosota?,
Mwanamuziki huyu aliongea mbele ya Naibu Waziri wa
Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Amos Makalla kwa uchungu mkubwa
huku akimtaka Yustus Mkinga akane mbele yake.
Bahati Bukuku akielezea namna alivyokamata kazi
zake nchini Zambia, akidai watu hao wanafahamiana na Mkinga waliyempigia
simu akawatetea.
Alidai akiwa Mbeya alikamata na kumpeleka
mtuhumiwa polisi, lakini hali ilikuwa ileile na alivyorudi Cosota
hakusikilizwa zaidi ya kupuuzwa na kuelezwa maneno ya kejeli.
Kinachonipa wasiwasi hapa ni tamko la wasanii,
kwamba endapo watashindwa kufanya hivyo ndani ya kipindi kifupi Chama
cha Waigizaji wa Filamu Tanzania (TDFAA), kitaitisha maandamano ya
wasanii nchi nzima.
na yatafanyika mfululizo.
Wasanii hawa wanasema wanamshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa
jitihada zake za kuongeza ajira kwa vijana, hivyo wangependa kuona
mamlaka za sanaa nchini nazo zinaunga mkono.
Wanasema huo ndiyo msingi wa malalamiko yao, Ofisi
ya Bodi haitoi ushirikiano katika hoja zao, mtazamo wa kiongozi
mtendaji ni kuvuna pesa tu.
Namnukuu Mwenyekiti wa TDFAA, Michael Sangu
“Katika hali ya kusikitisha kwa nyakati tofauti ikiwemo katika msiba wa
msanii mwenzetu, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Katibu Joyce Fisoo amekuwa
akiwaambia baadhi ya wasanii kwamba ‘mnajisumbua hakutakuwa na
mabadiliko yoyote ya gharama katika kanuni za filamu, hivyo
msihangaike’,” alisema.
Alidai Joyce amekuwa mmoja wa watendaji wa
Serikali wasiowatakia mapenzi mema wasanii na kwamba ushahidi upo wa
kutosha ikiwemo katika vikao kadhaa mtendaji huyo amekuwa akiwapuuza.
Suala hili ni nyeti linalotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi ili kuweza kuiweka sekta ya sanaa katika hali nzuri.
No comments:
Post a Comment