Taarifa kutoka mji wa Suez, Misri, zinaeleza kuwa ofisi ya usalama ya serikali imechomwa moto.
Hayo yametokea wakati maelfu ya watu
wakipita mabara-barani kwenye mhadhara wa mazishi ya wale waliokufa
katika mapambano ya Ijumaa - siku ya kuadhimisha miaka miwili ya kuanza
ghasia zilizomuangusha Rais Hosni Mubarak.
Wanajeshi wa serikali wanaendelea kupiga doria mjini Suez.
Watu kama 10 walikufa katika ghasia za Ijumaa.
Mjini Cairo, mapambano piya yamezuka kati ya askari polisi na waandamanaji karibu na wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Misri.
Polisi walifyatua moshi wa kutoza machozi kujaribu kuwazuwia waandamanaji wasifike kwenye jengo la wizara.
No comments:
Post a Comment