MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za injili nchini, Bony Mwaitege,
anatarajiwa kuupamba uzinduzi wa albamu ya ‘Baraka Huja’ ya Baraka
Legembo, utakaofanyika ndani ya Kanisa la Pentecoste Holiness Mission
lilipo Changanyikeni jijini Dar es Salaam, Januari 27, mwaka huu.
Akizungumza jana, Legembo
alisema kuwa Mwaitege amekubali kuimba katika uzinduzi huo unaotarajiwa
kuanza majira ya saa 7:00 mchana mara baada ya ibada.
“Mwaitege amekubali kuja kwenye uzinduzi wa albamu yangu, hivyo
nawaomba wakazi wote wa Changanyikeni kufika kwa wingi katika shughuli
hiyo itakayoanza saa 7:00 mchana, mara baada ya ibada,” alisema Legembo.
Legembo aliwataja waimbaji wengine watakaoimba siku hiyo kuwa ni kwaya
wenyeji, Elshadai Aliko Mwandelile, Ipyana Wasoto, Linus, Hanston,
Eliza, Neema, Kwaya ya Lulu na Mount Herob.
Aidha, alisema kuwa lengo la uzinduzi huo ni kupata fedha ambazo
zitamsaidia katika kurekodi albamu hiyo katika mfumo wa video, kwani
watu wengi wamekuwa wakiisubiri kwa muda mrefu.
“Lengo la kuzindua albamu yangu ni kupata fedha ambazo zitanisaidia
kurekodi albamu hii katika mfumo wa video, kwani watu wengi wamekuwa
wakiiulizia kila ninapokwenda kuhudumu,” alisema Legembo.
Aliongeza kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo atamtangaza siku za hivi karibuni, hivyo wadau wote wafike bila kukosa.
No comments:
Post a Comment