Mwalimu
wa Shule ya Msingi Nguruka Mkoa wa Kigoma, Helman Gabriel Masengi (30),
amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kigoma kujibu shitaka la
kughushi barua kuwa ameteuliwa kuwa Afisa Taaluma wilayani Chato, Mkoa
wa Geita.
Mshitakiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, David Ngunyale, kwa kosa la kughushi barua kuwa ameteuliwa kuwa Afisa Taaluma.
Mwendesha Mashitaka, Ochieng Asiago, alidai kuwa Julai 25, mwaka 2011 majira ya mchana katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, mshitakiwa alipeleka barua kwa Afisa Utumishi wa halmashauri hiyo kuwa ameteuliwa kuwa Afisa Taaluma wa Wilaya ya Chato.
Asiago aliendelea kudai kuwa baada ya kuwasilisha barua hiyo, mshitakiwa alikwenda kuripoti Chato na kwamba alipofika huko walikataa kumpokea kwa maelezo kuwa barua yake ya uteuzi ilikuwa ya kughushi.
Mshitakiwa huyo alikana shitaka na yuko nje kwa dhamana. Hata hivyo, upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali.
Hakimu Ngunyale alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 12, mwaka huu kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment