Wanafunzi 13,275 wamekacha kujiunga sekondari za kata katika Manispaa ya
Kinondoni kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, imefahamika.
Sababu kubwa iliyowafanya wazazi na walezi kutowapeleka watoto wao katika shule hizo zimeelezwa kuwa ni kutokana na kutokuwa na imani na viwango vya elimu vinavyotolewa na shule hizo zinazomilikiwa na wananchi chini ya usimamizi wa halmashauri kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Taarifa ya Afisa Elimu Sekondari Kinondoni, Omath Sanga, iliyotumwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni na NIPASHE kuona nakala yake, inaonyesha kuwa mwaka 2010, wanafunzi 5,112 waliachana na shule hizo kati ya 15,700 waliochaguliwa, huku waliojiunga na shule hizo wakiwa ni 9, 487 tu.
Sanga alisema mwaka 2011, wanafunzi 14,823 walichaguliwa kuanza kidato cha kwanza, lakini walioitikia na kusoma shule hizo walikuwa 10,128 na 9,695 hawakuripoti katika shule hizo.

Taarifa ilisema mwaka jana, jumla ya wanafunzi 13,955, walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shule za kata katika Manispaa ya Kinondoni, lakini walioripoti walikuwa ni 9,487 huku 4,468 wakingia `mitini'.
Kufuatia hali hiyo, Manispaa ya Kinondoni imesema ina uhakika wanafunzi 13,804 waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka huu wa 2013 kati ya wote 14,520 watapata nafasi.
Afisa Uhusiano wa Manipaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera, aliliambia NIPASHE kuwa shule za kata za manispaa hiyo, zina jukumu la kupokea wanafunzi 13,804 kwa sababu wanafunzi 666 wamepokelewa mkoani, tisa ngazi ya taifa baada kupata ufaulu wa juu, 23 watasoma bweni ufundi na 18 bweni kawaida.
"Vijana wote watasoma katika shule zetu 46, ambapo kati ya hizo nane za kidato cha tatu na 38 zilikuwa na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana hivyo kuacha madarasa 150 yakiwa tupu huku vyumba vingine 32 havitumika mwaka jana," alisema.
Hata hivyo, Mhowera alisema inawezekana Manispaa ikawa na kazi ya ziada itakapokea wanafunzi wa awamu ya pili (second selection).
No comments:
Post a Comment