TAARIFA YA KUWASHUKURU WATANZANIA KWA USHIRIKI WAO KATIKA HATUA ZOTE
ZA MARADHI MPAKA KIFO NA MAZISHI YA MDAU MAREHEMU SAIDI JUMA KILOWOKO –
SAJUKI.
Ndugu Waandishi wa vyombo vya habari
Awali Shirikisho la Filamu Tanzania, TAF, linawapongeza Waandishi wote kwa jitihada na ushirikiano mkubwa mnaouonesha kwa TAFF katika kuripoti shughuli na matukio yanayohusu tasnia ya Filamu nchini na Shirikisho kwa uwazi na weledi mkubwa katika kuihabarisha jamii ya Watanzania mambo mbalimbali yanayohusu tasnia na Wasanii kwa ujumla.
Ndugu Waandishi wa vyombo vya habari
Awali Shirikisho la Filamu Tanzania, TAF, linawapongeza Waandishi wote kwa jitihada na ushirikiano mkubwa mnaouonesha kwa TAFF katika kuripoti shughuli na matukio yanayohusu tasnia ya Filamu nchini na Shirikisho kwa uwazi na weledi mkubwa katika kuihabarisha jamii ya Watanzania mambo mbalimbali yanayohusu tasnia na Wasanii kwa ujumla.
Ndugu Waandishi ikumbukwe kuwa mnamo mwanzoni mwa mwezi Septemba 2011 Shirikisho la filamu Tanzania lilipokea rasmi taarifa za ugonjwa wa Msanii ambaye pia ni Muongozaji katika kampuni ya Wajey Film Saidi Jumaa Kilowoko aliyejulikana zaidi kwa jina la SAJUKI.
Ambaye alikuwa amelazwa katika hospital ya TMJ Mikochein Dar es Salaam akisumbuliwa na tatizo la tumbo.
Ndugu Waandishi kwa mujibu wa taarifa za kidaktari Sajuki alitakiwa
kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi, katika kufanikisha matibabu
hayo nchini India, Shirikisho la Filamu Tanzania ikishirikiana na Wadau
mbalimbali wa Sanaa hapa nchini, Viongozi mbalimbali wa vyama na
Serilaki, Wafanyibiashara kutoka kada tofauti za biashara kwa pamoja
katika namna tofauti waliweza kuchangia gharama za safari hiyo,ambapo
zaidi ya Tshs 32 milioni zilipatikana.
Hali ya Sajuki ilirejea katika matumaini baada ya kurudi India ingawa
alitakiwa kurudi tena baada ya miezi mitatu kwa ajili kukamilisha tiba
,Tukiwa katika maandalizi ya kumrudisha India kwa matibabu, mwezi
Disemba 2012 hali ya SAJUKI ilibadilika ghafla ambapo alipelekwa
Hosptali ya Taifa Muhimbili na ikagundulika kuwa na upungufu mkubwa wa
Damu na kansa ya ngozi. Wasanii na wadau mbalimbali waliitikia wito wa
kuchangia damu na ilipatikana kama ilivyohitajiwa.
.
.
Ndugu Waandishi Wahenga walinena kwamba jitihada haziishindi kudra ya
Mwenyeezi Mungu mpaka 02 Januari 2013 Saidi Juma Kilowoko alifariki
dunia.
Kifo cha marehemu Sajuki kilivuta hisia za Watanzania wengi hasa
kutokana na historia ya maradhi kwa muda mrefu, aidha Shirikisho la
Filamu Tanzania,TAFF,linawashukuru Watanzania wote ambao waliweza
kushiriki kwa hali na mali wakati wa kipindi chote cha maradhi mpaka
umauti, hatuwezi kumkumbuka kila mmoja kwa nafasi yake.
.
.
Pamoja na hayo shukrani zimuendee Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr Mrisho Jakaya Kikwete kwa kufuatilia kwa ukaribu
maendeleo ya afya yake mpaka siku ya mazishi, pia tunawashukuru
Viongozi wa Shirikisho la Muziki, Shirikisho la Sanaa za Ufundi,
Viongozi wa vyama vya Siasa, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa vyama vya
Wasanii,vyombo vya habari, ndugu na jamaa wa familia ya marehemu kwa
ushirikiano waliouonesha kwa marehemu SAJUKI.
Tunajua hatuna cha kuwalipa lakini tunathamini michango yenu katika kumuuguza na mpaka siku ya kifo chake.
Shirikisho la Filamu Tanzania tunaomba jamii ya Watanzania kuendelea
kushirikiana na Wasanii katika Nyanja tofauti, lakini pia tunaomba
vyombo vya habari viendelee kutoa habari zinazohusu tasnia ya filamu
ambazo zitaonya, kuelimisha na kukumbusha wajibu wa Wasanii katika jamii
kwa maendeleo ya Taifa letu.
Tunaomba Mwenyeezi Mungu awafariji na kuwapa moyo wa subira Wastara,
Wazazi, ndugu na jamaa zake katika kipindi hiki kigumu na majonzi.
Hatuna cha kufanya zaidi kwa marehemu Sajuki ila ni kumuombea dua kila tunapomkumbuka.
Hatuna cha kufanya zaidi kwa marehemu Sajuki ila ni kumuombea dua kila tunapomkumbuka.
Tunamuomba Mwenyeezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi
AAMINI.
Ahsante kwa Ushirikiano.
SIMONI MWAKIFWAMBA
SIMONI MWAKIFWAMBA
RAIS.
No comments:
Post a Comment