EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, January 23, 2013

Taarifa ya Waziri: Wakala wa Kusimamia uendelezaji wa Mji Mpya, Kigamboni

Picture
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africajijini Dar es salaam leo wakati alipotangaza rasmi kuanzishwa kwa Wakala wa kusimia maendeleo ya mji wa Kigamboni inayoitwa Kigamboni Development Agency (KDA) Kushoto ni Christian Mwangaja Kaimu Kamishna mambo ya Ardhi na katikati ni Sellasie Mayunga Upimaji na Ramani.

1. Serikali imedhamiria kujenga Mji Mpya Kigamboni katika Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, Dhana ya mji mpya Kigamboni ni kuwa na mji wa kisasa ambao ni kitovu cha kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika jiji la Dar es Salaam ili liweze kushindana na miji mingine duniani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii na kukuza ajira, hasa kwa vijana. Ujenzi wa mji mpya ni hatua mojawapo katika mkakati wa serikali wa kukabiliana na changamoto za ukuaji wa jiji la Dar es Salaam.

 2. Tarehe 18 January, 2013 Serikali ilianzisha kisheria wakala maalumu, Kigamboni Development Agency (KDA) itakayosimamia uendelezaji wa Mji Mpya Kigamboni kama Mamlaka ya Upangaji Mji (Planning Authority). Eneo litakalosimamiwa na KDA lina ukubwa wa hekta 50,934 na linahusisha Kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila, Kisarawe II, Kimbiji na Pemba Mnazi . katika kusimamia uendelezaji huo, KDA itaongozwa na mpango kabambe. Rasimu ya mpango huo imekwisha andaliwa kwa baadhi ya kata. 3. Uendelezaji wa Mji Mpya utagharimiwa na Serikali pamoja na sekta binafsi kwa kutumia fedha zilizo ndani na nje ya bajeti rasmi ya serikali. Utaratibu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (Public Private Partnership) utatumika. Aidha, mbinu za kisasa za kupata fedha kama vile kuuza hisa na kutoa hatifungani (bonds) zitatumika.

4. Ili kutekeleza kusudio la kuendeleza eneo la Kigamboni, hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na:-
  • Kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa ya kuendeleza eneo la Kigamboni na taratibu za uendelezaji.
  • Kutafuta fedha za kutosha kutekeleza mradi.
  • Kupima maeneo husika na kuyaandaa kwa ajili ya uendelezaji.
  • Kujenga nyumba mpya za kuishi kwa ajili ya kuwahamishia wananchi ambao makazi yao yataathiriwa na ujenzi wa Mji Mpya; na
  • Kufanya uthamini wa mali na kuwafidia wananchi watakaolazimika kahama kutokana na ujenzi wa mji.

5. Muundo wa KDA unatokana na Sheria ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997. wakala itaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji na Wakurugenzi sita ambao watakuwa Wakuu wa Idara, KDA itasimamiwa na Bodi ya Ushauri pamoja na Baraza la Ushauri ambalo  litakuwa na wajumbe wanaowawakilisha wadau wote, hususan Wabunge na Madiwani waeneo litakaloendelezwa na KDA.

6. Matokeo ya utekelezaji wa Mpango kabambe wa Mji Mpya ni kama ifuatavyo:
  • Kuwa na mji uliopangwa kwa kiwango cha kimataifa utakaokuwa mfano wa kuigwa na miji mingine nchini.
  • Kupunguza ujenzi holela;
  • Kuongeza mapato ya serikali yanayotokana na shughuli za kiuchumi na kijamii kama vile za viwanda , hoteli, utalii, biashara, elimu, ofisi, afya na vituo vya michezo;
  • Kupunguza msongamano wa magari na huduma za kiuchumi na kijamii katikati ya jiji la Dar es Salaam;
  • Kuongezeka kwa thamani ya ardhi katika maeneo ya mji kutokana na kuboreshwa kwa miondombinu ya barabara, maji na umeme itakayowezesha kukuza biashara, ujenzi wa majengo na viwanda.
  • Kuhamasisha uwekezaji ili kuongeza ajirra, has kwa vijana; na
  • Wananchi  wengi wataweza kumiliki nyumba katika maeneo yaliyopangwa na kutumia nyumba zao kupata mikopo kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali.
Taarifa na elimu kwa umma kuhusu hatua zote za uendelezaji wa mji  zitaendelea kutolewa na Wizara pamoja na KDA kwa njia mbalimbali (k.m. kupitia mikutano maalum, vyombo vya habari na vipeperushi).

 Prof. Anna K. Tibaijuka (Mb)
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
23 January, 2013

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate