Timu ya Young Africans Sports Club imeendeleza wimbi lake la
ushindi baada ya kuichapa timu ya Black Leopard ya Afrika Kusini mabao
2-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza.
Mashabiki wakiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia uwanjani.
Kikosi cha kocha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza
mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la mapema, kwani timu ya Black
Leopard nayo leo iliingia ikiwa na dhamira ya kupata ushindi na kuondoa
hali ya kufungwa mara ya pili na Young Africans.
Kikosi cha timu ya Black Leopards.
Iliwachukua
watoto wa jangwani dakika 3 tu kujipatia bao la kwanza lililofungwa na
mshambuliaji Said Bahanuzi kwa kichwa akimalizia mpira uliopigwa na
Kabange Twite na kugonga mtambaa wa panya kabla ya kumkuta mfungaji
Bahanuzi aliyeukwamisha mpira wavuni.
Black
leopard iliibadilika na kucheza kwa kasi ili kusaka bao la kusawazisha
na katika dakika ya 12, mshambuliaji wa Black Leopard Joshua Obaje
aliipatia timu yake bao la kusawazisha kufuatia uzembe wa walinzi wa
Yanga waliozembea kumkaba mfungaji huyo aliyepiga shuti kali na mpira
kutinga wavuni.
Timu zote zilicheza soka la
kushambuliana kwa zamu na nusra Bahanuzi tena aipatie Young Africans bao
la pili lakini umakini wa mlinda mlango Postentt Omony aliweza kuokoa
mchomo huo na kutoka nje kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 1- 1.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo kocha
Brandts aliwatoa Kabange Twite, Nurdin Bakari, David Luhende, Said
Bahanuzi, Hamis Kiiza na nafasi zao kuchukuliwa na Haruna Niyonzima,
Athumani Idd, Jerson Tegete, Frank Domayo na Didier Kavumbagu.
Young
Africans ilibadilika sana uchezaji na hasa eneo la kiungo ambapo Frank
Domayo, Haruna Niyonzima na Athumani Idd waliweza kuwafunika kabisa
viungo wa timu ya Black Leopard.
Dakika ya 53
Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la pili kwa mkwaju wa penati
kufuatia mlinzi wa Black Leopard Vicent Mabwisela kumchezea ndivyo sivyo
mshambuliaji wa Young Africans Didier Kavumbagu na Tegete kuukwamisha
mpira huo wavuni.
Yanga iliendelea kulishambulia
lango la Black Leopard kwa dakika zote za kipindi za kipindi cha pili na
kama washambuliaji wake Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na Saimon Msuva
wangekua makini timu ingeibuka na ushindi wa mabao mengi.
Black
Leopard iliendelea kucheza kwa nguvu kusaka bao la kusawazisha lakini
umakini wa walinzi Yanga ilikuwa kikwazo kwao kuweza kupata bao la
kusawazisha.
Dakika
ya 89, Kelvin Yondani alitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Alex
Mahagi baada ya kumchezimu ya ea madhambi mshambuliaji wa timu ya Black
Leopard.
Golikipa wa timu ya Black Leopards,Posnett Omony akisota kuokoa mpira
uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete kwa
njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele
mpaka dakika 90kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye
mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa
CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 2- 1 Black Leopard.
Kocha
mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kwa kupata
ushindi huo wa leo, kwani timu ya Black Leopard ni timu nzuri,naleo
ilingia kucheza kwa nguvu ili ipate ushindi na kufuta uteja dhidi ya
Yanga lakini mwisho wa siku vijana wangu walikuwa ni bora zaidi ndio
maana wameibuka na ushindi huo.
Kambi yetu ya
mafunzo nchini Uturuki imetusaidia sana, wachezaji wanacheza kwa
kujiamini wametulia hawana presha ya mchezo, hali inayopelekea kucheza
migongeano kwa uhakika na hii ni dalili tosha kuwa tupo tayari kwa
mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom alisema 'Brandts'
Naye
kocha wa Black Leopard Abel Makhubele amesema timu yake leo ilicheza
vizuri sana na kwa uelewano mkubwa, kwani hivi sasa wachezaji wake
wamezoea hali ya hewa na mazingira, lengo letu likikuwa ni kuibuka na
ushindi katika mchezo wa leo lakini makosa yaliyojitokeza kwa safu yetu
ya ushindi ndiyo yaliyopelekea mchezo huu wa leo.
Hii
ilikuwa ni mechi ya pili kucheza kwa Young Africans dhidi ya Black
Leopard ambapo katika michezo yote Yanga imeibuka na ushindi wa mabao
3-2 katika mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam na ushindi wa mabao 2-1
katika mchezo wa leo
Young
Africans itafanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya
kuanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam majira ya mchana kwa
shirika la ndege la Fast jest ambapo inatarajiwa kufika maira ya saa
12:30 jioni.
Young Africans: 1.Ally
Mustapha 'Barthez', 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir
Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Nurdin Bakari/Athuman Idd
'Chuji', 7.Saimon Msuva/Nizar Khalfani, 8.Kabange Twite/Frank Domayo,
9.Said Bahanuzi/Didier Kavumbagu, 10.Hamis Kiiza/Jerson Tegete, 11.David
Luhende/Haruna Niyonzima
Black Leopard:
1.Posnett Omony, 2.Moses Kwena, 3.Thulani Ntishineila, 4.Vicent Mabsela,
5.Victor Kamhuka/Sizwe Sibiya, 6.Bafana Sibeko, 7.Tiyane
Mabunda/Sphamandla Sibaiya, 8.Michael Nkabule/Raymond Monana, 9.Joshua
Obaje/Mxolisi Gunede/, 10.Mondli MiyaThabo Mongalo, 11.David Zulu/Tommy
Mandalazi
No comments:
Post a Comment