Timu
ya Young Africans ambayo ilikuwa imeweka kambi ya mafunzo takribani
wiki mbili mjini Antlaya nchini Uturuki kesho siku ya jumamosi itashuka
dimba la Uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Black
Leopard kutoka nchini Afrika Kusini.
Black Leopard timu inayoshiriki ligi kuu ya Afrika
Kusini maarufu kama PSL inatazamiwa kuwasili mchana huu kwa shirika la
ndege la South African Airways ikiwa na msafara wa watu 42, ambapo timu
pamoja na viongozi wake watafikia katika hotel ya White Sands Mbezi
Beach.
Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga
tangu kurejea nchini, hivyo ni nafasi kwa wadau, wapenzi wa soka kufika
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuweza kujioniea mchezo huo
majira ya saa 10 jioni siku ya jumamosi.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata
nafasi ya kucheza na timu kutoka katika ligi kuu ya PSL nchini Afrika
Kusini hivyo atatumia nafasi hvyo kukamilisha maandalizi ya mzunguko wa
pili wa ligi kuu ya Vodacom.
Leo asubuhi Young Africans imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Mabatiini Kijitonyama tayari kabisa kujianda na mchezo huo.
Wachezaji wote wameendela na mazoezi leo isipokuwa Hamis Kiiza 'Diego' na mlinda mlango Yusuph Abdul ambao wanaoumwa malaria.
Aidha
katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako amemtambulisha Dr Nassoro
Matuzya kwa wachezaji leo asubuhi kama dakatari wa timu ambapo ameanza
kazi kushika nafasi ya daktari aliyekuwepo Dr Suphian Juma.
No comments:
Post a Comment