ARSENAL
wanaelekea ukingoni mwa michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kipigo
cha 3-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Bayer Munich ya
Ujerumani.
Bayern waliwasambaratisha vijana wachovu wa Wenger kupitia mabao ya Toni Kroos, Thomas Muller na Mario Mandzukic.
Shangwe za mashabiki wa Bayern
Hata
pale Podolski alipoipunguzia Arsenal bao dakika ya 55 na kuwa 2-1 bado
ilionekana Arsenal wana mlima mrefu wa kupanda ili kushinda mechi ya
marudiano ugenini.
Podolski akiifungia Arsenal bao pekee
Vijana
wa Wenger walibakiwa na tumaini pekee katika ligi ya mabingwa baada ya
kutolewa na Blackburn kwenye kombe la FA Jumamosi iliyopita.
Walianza kupumbazwa dakika ya nane pale Kroos alipoujaza mpira wavuni kupitia krosi ya Thomas Muller.
Kroos (kushoto) baada ya kufunga bao la kwanza
Dakika
ya 21 mambo yakawa mabaya zaidi baada ya mpira wa kona wa Daniel Van
Buyten kutemwa na kipa Szczesny na kumkuta Muller aliyeujaza wavuni na
kuandika bao la pili.
Muller akiipatia Bayern bao la pili
Bayern
Munich ikapigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Arsenal dakika ya
77 baada ya Mandzukic kumalizia mpira wa krosi ya Arjen Robben
aliyetokea benchi.
Katika mchezo mwingine, Porto iliifunga Malaga 1-0.
Chanzo saluti5
No comments:
Post a Comment