EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, February 19, 2013

Askofu Shao, ndugu wa Padri Mushi walia na Serikali

ASKOFU wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Zanzibar, Augustino Shao na ndugu wa marehemu wa Padri Evarist Mushi wameitupia lawama Serikali kwa kuzembea kuwalinda viongozi wa dini hiyo waishio Zanzibar licha ya kupewa taarifa za viashiria vya hatari mara kwa mara.Askofu Shao alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar na ndugu wawili wa Padri Mushi walieleza hayo huko Moshi.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana kwamba hawajapata malamamiko yaliyoelezwa na Askofu Shayo na kwamba kama Rais Jakaya Kikwete angeyapata asingeacha kuyashughulikia.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa naye alikanusha madai hayo akisema:
“... Hapa tulipo tuna kesi nyingi na kuna watu wanahojiwa. Sisi hatufanyi kazi kwa shinikizo la mtu, kama ni hivyo vipeperushi hata sisi tunavipata siyo wao tu. Sasa tutawakamataje wakati watu wenyewe hatuwajui?”
Hata hivyo, Askofu Shao alisema hawaridhishwi na utendaji kazi wa Polisi na kudai kwamba Wakristo wa madhehebu yote wanalengwa na mashambulio yanayofanywa na watu aliosema kuwa wanapata msaada kutoka nje.
“Niseme wazi tu, haturidhishwi na utendaji wa Serikali katika kutulinda. Tumemwandikia barua Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Rais Jakaya Kikwete tukiwaeleza vitisho tunavyopewa, lakini hatuoni hatua zikichukuliwa,” alisema Askofu Shao na kuongeza:
“Walipomshambulia Padri Ambrose Mkenda watu hao walileta ujumbe kwamba, tumeshawaweza Padri Ambrose na Sheikh Fadhil Soraga na bado tutaendelea. Vijana wetu wa kazi wameshamaliza mafunzo Somalia,” alinukuu moja ya kipeperushi huku akisema kuwa tatizo la Serikali ni kutokuwajibika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alikiri kupokea taarifa hizo za vitisho na kusema Serikali ina vyombo na taratibu zake katika kufanya kazi... “Sasa unataka Rais akamate wahalifu? Nadhani mtu sahihi wa kuzungumzia mambo haya atakuwa Kamishna wa Polisi. Ni kweli taarifa zimeletwa lakini nasi tulizipeleka kwenye vyombo vinavyohusika navyo ni Polisi.”


Askofu Shayo aliisifu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisema imejizatiti... “Bara wana nguvu, mtu akifanya kosa leo anakamatwa, lakini Zanzibar wanafanya kazi kwa kujuana.”


Askofu huyo alipinga kauli ya Serikali kuwa itahusisha taasisi za kimataifa kuwasaka wahusika wa mauaji akisema Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) likishirikiana na wananchi wanaweza kupata suluhu.


“Jeshi halijashindwa kumaliza uhalifu huu. Ukileta askari wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) watashindwa tu kwani hata Kiingereza hakitaeleweka. Bado watahitaji kupata msaada wa wananchi. Serikali inawajua wanaohusika, wanajua wanakokaa, tatizo ni uwajibikaji,” alisema Askofu Shao.


Hata hivyo, alisema kuwa hana ugomvi na Waislamu, bali anatofautiana na watu wote, wakiwamo Wakristo wanaotumia mgongo wa dini kufanya vurugu za kidini.
Askofu wa Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pengo alisema kuwa mauaji ya Padri Mushi yangeweza kuzuiliwa kama viongozi wa nchi wangesoma alama za nyakati.


Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana Kadinali Pengo alisema ni muhimu viongozi wa nchi kuchukua hatua na kuzuia yanayotokea na kuhusisha dini fulani.
Akimzungumzia marehemu Padri Mushi, Askofu Shao alisema: “Alikuja hapa Zanzibar tangu alipokuwa na miaka 18 akiwa anasoma elimu ya sekondari.

Mazishi yake
Askofu Shao alisema kuwa Ibada ya Mazishi ya Padri Mushi itafanyika Jumatano katika Parokia ya St. Joseph, Minara Miwili, Zanzibar na mwili wake utazikwa eneo la Kitope wanakozikwa viongozi wa kanisa.

“Padri Mushi ameishi Zanzibar tangu akiwa na miaka 18 hivyo ni mkazi wa Zanzibar. Hakuna sababu ya kusafirishwa. Ukishakuwa padri unakuwa mali ya kanisa. Nimesikia kuna ndugu zake wanadai mali wengine wanasema eti alikuwa na gari... hii ni mali ya kanisa.”


Ndugu wanena
Mdogo wa marehemu Padri Mushi ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Majengo ya Mjini Moshi, Benedict Mushi alisema kaka yake alimweleza kuwa amekuwa akitishiwa kuuawa na watu wasiojulikana.
“Mara ya mwisho alikuja hapa nyumbani akaniambia bado anaendelea kupata vitisho vya kuuawa kupitia ujumbe wa simu na alinionyesha meseji alizokuwa akiandikiwa kutishiwa,” alisema.
Mwalimu huyo alisema vitisho hivyo vilikuwa na sura mbili, moja vikihusiana na masuala ya dini na nyingine vilikuwa vikihusiana na masuala ya ubara kwa maana alikuwa hatakiwi Zanzibar.
“Mara zote nilimshauri atoe taarifa polisi na yeye aliniambia alishatoa taarifa polisi kwa hiyo nafikiri wakifuatilia hizo simu na meseji wanaweza kuwabaini hao wauaji,” alisema mwalimu huyo.
Kaka mkubwa wa padri huyo, Adolf Mushi alisema aliwahi kumshauri marehemu ahame Zanzibar lakini alikataa na wakakosana.
“Nilishatazama hali ya mambo kule Zanzibar hasa baada ya yule padri mwingine kupigwa risasi nikamwambia hivi huwezi kutoka huko, akasema hawezi kuwaacha kondoo wake,” alisema.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate