EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, February 19, 2013

SHULE ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI SOMA HAPA

Tafadhali tizama matokeo hayo kwa ku:
ILANI:  


- Linki moja isipofunguka, jaribu nyingine, rudia tena na tena. Pia refresh page.  
- Matokeo yote yapo kwenye tovuti ya NECTA (www.necta.go.tz). Ifahamike kuwa wavuti.com503 Service Temporarily Unavailable error hai-host wala haihusiki na kushindwa kufungua linki zilizotajwa hapo juu kwa na matatizo ya server na 503 Service Temporarily Unavailable error za NECTA kuishiwa bandwidth kwa kuelemewa na wingi wa watembeleaji/requests wanaotaka kutizama matokeo hayo.

1.0                 UTANGULIZI
Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012.  Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :
2.0                 MTIHANI WA MAARIFA (QT)

2.1           Usajili na Mahudhurio

Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni8,176Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani. 

2.2          Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)

Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).

3.0                 MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012

Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.

3.1                 Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa

(a)           Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 480,036 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia54.67.  Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012  ni 456,137 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa21,820 sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani.

(b)            Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 411,230 wakiwemo wasichana 182,978 sawa na asilimia 44.50 na wavulana228,252 sawa na asilimia 55.50.  Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani walikuwa 397,136 sawa na asilimia96.57. Aidha, watahiniwa 14,090 sawa na asilimia 3.43hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro,  ugonjwa na vifo.

(c)             Watahiniwa wa Kujitegemea

Watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni68,806 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia 49.71.Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917 nawavulana 30,084  wamefanya mtihani wakati watahiniwa7,730 sawa na asilimia 11.23  hawakufanya mtihani.

4.0                 MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(a)                 Watahiniwa wa Shule
Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya watahiniwa397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni 80,686.

(b)                Watahiniwa wa Kujitegemea

Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 16,112kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani.  Wasichana waliofaulu ni 6,751 na wavulana ni 9,361

5.0                 UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI

Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,520 wamefaulu katikamadaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni 7,178 na wavulana ni16,342.

Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:

DarajaIdadi ya WavulanaIdadi ya WasichanaJumla
I1,0735681,641
II4,4561,9976,453
III10,8134,61315,426
I-III16,3427,17823,520
IV64,34438,983103,327
0120,664120,239240903

6.0        SHULE ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI

Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5.  Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule ya kwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :

NAFASIJINA LA SHULEIDADI YA WATAHINIWAMKOA
1ST. FRANCIS GIRLS90MBEYA
2MARIAN BOYS S.S75PWANI
3FEZA BOYS S.S69DAR ES SALAAM
4MARIAN GIRLS S.S88PWANI
5ROSMINI  S S78TANGA
6CANOSSA S.S66DAR ES SALAAM
7JUDE MOSHONO S S51ARUSHA
8ST. MARY’S MAZINDE JUU83TANGA
9ANWARITE GIRLS S S49KILIMANJARO
10KIFUNGILO GIRLS S S86TANGA
11FEZA GIRLS49DAR ES SALAAM
12KANDOTO SAYANSI GIRLS SS124KILIMANJARO
13DON BOSCO SEMINARY SS43IRINGA
14ST.JOSEPH MILLENIUM133DAR ES SALAAM
15ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO SS64KIGOMA
16ST.JAMES SEMINARY SS44KILIMANJARO
17MZUMBE SS104MOROGORO
18KIBAHA SS108PWANI
19NYEGEZI SEMINARY SS68MWANZA
20TENGERU BOYS SS76ARUSHA


7.0        SHULE KUMI AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI

NAFASIJINA LA SHULEIDADI YA WATAHINIWAMKOA
1MIBUYUNI S.S40 LINDI
2NDAME  S.S41UNGUJA
3MAMNDIMKONGO S.S63PWANI
4CHITEKETE S.S57MTWARA
5MAENDELEO S.S103DAR ES SALAAM
6KWAMNDOLWA S.S89TANGA
7UNGULU S.S62MOROGORO
8KIKALE S.S60PWANI
9NKUMBA S.S152TANGA
10TONGONI S.S56TANGA


8.0           TATHMINI YA UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012


8.1           Tathmini ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Aidha, shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:


(i)         Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;


(ii)        Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea; na


(iii)       Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.


8.2           Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yafuatayo:


(i)             Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule. Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.


(ii)            Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.


(iii)           Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.


(iv)           Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.


(v)            Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo yao.

9.0           MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA


Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:


(a)           Watahiniwa 28,582 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada wanayodaiwa pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.


(b)           Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71 waliofanya Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.

10.0        MATOKEO YA MITIHANI  YALIYOFUTWA


10.1              Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Udanganyifu

Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo yao yote ya mtihani kwa mujibu wa kifungu Na.52(b) cha Kanuni za Mitihani baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba 2012. Kati yao, watahiniwa wa shule ni 624na watahiniwa wa kujitegema ni 148 na watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa (QT) ni 17.

Aina ya udanganyifu uliobainika na idadi ya watahiniwa husika ni kama ifuatavyo:

S/NAINA YA UDANGANYIFUIDADI YA WATAHINIWA
(i)       Watahiniwa kubainika kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika skripti ya somo moja au zaidi ya moja.04
(ii)      Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na ‘notes.’170
(iii)Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu.590
(iv)Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani ‘impersonation”.04
(v)      Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha mtihani.06
(vi)Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha karatasi za maswali au skripti kwa lengo la kufanya udanganyifu.15

JUMLA789

10.2              Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Watahiniwa Kuandika Matusi Katika Skripti Zao

(i)          Jumla ya watahiniwa 24 waliandika matusi kwenye skripti zao za masomo mbalimbali. Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5(13) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:


Written responses to any examination question which carry words, drawings or pictures connected to sex or abusive language in such a way that it becomes offensive shall consitute an examination offence and a candidate who commits such an offence shall be punished by the Council.”


Kutokana na kosa hilo Baraza la Mitihani limefuta matokeo yao yote kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2)(a) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka: 


A candidate found to have committed an examination offence shall - (a) have his examination results nullified”


(ii)         Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu (skripti) kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Serikali haitaweza kuwavumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo. Hivyo, Serikali itaangalia hatua zaidi za kisheria za kuchukua dhidi ya watahiniwa wote walioandika matusi.


Kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2)(b) cha Kanuni za Mitihani, watahiniwa wote waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani au kuandika matusi katika skripti zao hawataruhusiwa kufanya mitihani inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania  kwa kipindi cha mwaka mmoja (01) kuanzia tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.



11.0        KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA CSEE na QT, 2012


(a)           Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2012  yanapatikana katika tovuti zifuatazo:


(b)           Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya  ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:


MATOKEOXNAMBA YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA


(Mfano : matokeoxS0101x0503)



Dkt.  Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate