NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinum’, amewajibu baadhi ya wadau wa muziki wa kizazi kipya ambao
wameandika katika mitandao ya kijamii kwamba msanii huyo ameishiwa
mistari na anaelekea kuachana na mambo ya muziki.
Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinum
Akizungumza katika kipindi cha sports extra kinachorushwa na Redio
Clouds jijini Dar es Salaam juzi, Diamond alisema Mungu ndiye anayejua
mwisho wake na sio binadamu wa kawaida.
“Mungu ndiye anayejua mimi nafanya nini na lini utakuwa mwisho wangu;
hao wanaoandika hivyo ni mitazamo yao, mimi siwezi kuwazuia kwani baadhi
ya walimwengu huwa hawapendi maendeleo ya wenzao na ndio maana mimi
naachia kazi mfululizo ili kuwaziba midomo yao,” alisema Diamond.
No comments:
Post a Comment