MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinum’ amewalalamikia watu waliomuibia simu yake na kuvujisha wimbo
wake mpya ambao anatarajia kuuachia hivi karibuni.
Akielezea jinsi wimbo huo ulivovuja jijini Dar es Salaam jana, Diamond
alisema nyimbo zake huwa anazitunza katika simu yake ya mkononi, hivyo
mara ilipoibiwa akasikia wimbo huo umeshanza kusikika mtaani.
“Wimbo unaitwa ‘Ukimuona’, ni kati ya nyimbo zangu ambazo zimesimama
na zenye maneno fulani ya kuwashika mashabiki, kiukweli mistari
imesimama, naandaa video yake, pamoja na kuvuja, nitaitoa hivyo hivyo
maana ni bonge la ngoma,” alisema Diamond.
Alisema kazi hiyo ataiachia wiki ijayo na kuwaomba mashabiki wake
wakae mkao wa kula, kwani anaamini mistari yake imesimama na ina ujumbe
katika jamii.
Diamond kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Kesho’ ambacho
kimeliteka soko la muziki mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vinafanya
vizuri.
No comments:
Post a Comment