MWIMBAJI
supa staa wa kizazi kipya, Naseeb Abdul “Diamond” amefunguka kuwa
hajawahi kusafiria nyota ya msanii mwenzake Q-Chillah.
Akiongea
katika kipindi cha XXL cha Clouds FM jana mchana, Diamond alisema
ameshangazwa na maneno ya Q-Chillah kuwa yeye (Diamond) anamloga na
kusafiria nyota yake.
“Hivi nimloge au kusafiria nyota yake ipi hiyo? …hii ya kula unga? Alihoji kwa hasira Diamond.
“Mimi
najituma, nafanya kazi kwa bidii, yeye anahangaika na mastarehe yake
hayo halafu anasema nasafiria nyota yake, kwa kipi haswa? Kwanza wakati
mimi naingia kwenye game Q-Chillah alishapotea,” aliongeza.
Diamond ndani ya studio za Clouds FM, jana mchana
Siku
kadhaa zilizopita, kupitia kipindi hicho hicho cha XXL, Q-Chillah
alimshambulia Diamond kuwa anamloga na kusafiria nyota yake.
Hata hivyo Diamond aliendelea kusisitiza kuwa bado ataendelea kumsheshimu Q-Chilllah kama msanii aliyemtangulia kwenye fani.
Diamond
pia alipuuza madai ya mtu anayepita kwenye vyombo vya habari kutangaza
kuwa ni mganga wake na kumtaka kama ni mganga kweli basi amshushe
kisanii.
Akizungumzia
madai ya kukosa watu kwenye show zake za Zanzibar na Mwanza, Diamond
alisema hizo ni fitna za wapinzani wake ambao huchukua picha za mapema
kabla show haijaanza na kuzitumia kama kilelezo cha kuanguka kwa show
zake.Via saluti5
No comments:
Post a Comment