BAADA ya kurejea uraiani, msanii wa filamu, Elizabeth Michael
‘Lulu’, baadhi ya watu wameibuka na kutumia jina lake na baadhi ya
wasanii katika mtandao wa kijamii wa Facebook kujipatia fedha kwa madai
msanii huyo anahitaji kusaidiwa.
Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Clouds FM,
msanii aliye karibu na familia ya Lulu, Mahsen Awadh ‘Dk. Cheni’,
alisema wametaarifiwa na watu wao karibu kuwa wamesoma ujumbe wao katika
Facebook kuwa wanaomba fedha kwa ajili ya Lulu kwa ajili ya kumsaidia
katika kesi inayomkabili.
“Mimi sijui nchi yetu inaelekea wapi, tunashindwa kumuombea mwenzetu
afikie pazuri badala yake tunatafuta njia ya kuiba kupitia matatizo ya
mtu; naomba nieleweke kwamba mimi siko katika mtandao wowote na wala
sijawahi kujiunga na mitandao hiyo, hivyo hao wanaotumia jina langu na
la Jokate ni matapeli wakubwa na kaeni nao mbali,” alisema Dk. Cheni.
Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya aliyekuwa
nguli wa filamu Tanzania, marehemu Steven Kanumba, Aprili 7 mwaka jana
nyumbani kwake Sinza, Vatican, ambapo alikuwa mahabusu hadi Januari 29
mwaka huu alipopata dhamana.
No comments:
Post a Comment