RAIS Jakaya Kikwete amekutana na wabunge na wadau wa Mkoa wa
Mtwara Ikulu ya Dodoma, huku kukiwa hakuna taariga ya kilichozungumzwa.
Jana, wabunge wa Mtwara walionekana Ikulu muda
mfupi baada ya Rais Kikwete kuingia mkoani Dodoma kuongoza kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM.
Waandishi wa habari waliokuwa wameitwa kwa Rais Kikwete kushuhudia makabidhiano ya Bajaj kwa Sarah Mkumbo, waliwaona wabunge hao wakiwa Ikulu.
Hivi karibuni kuliibuka matukio ya uvunjifu wa amani Mkoa wa Mtwara, ikiwamo upotevu wa mali na vifo vya watu kutokana na wananchi kupinga suala la kusafirisha gesi inayotarajia kwenda Dar es Salaam.
Kutokana na vurugu hizo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilazimika kwenda kuweka kambi mkoani Mtwara kwa siku mbili kukutana na makundi mbalimbali kwa ajili ya kuweka mambo sawa.
Baada ya Pinda kurudi, juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika kutafuta jinsi ya kuzima moto wa wananchi ambao wamekuwa wakikaririwa kwamba, wako tayari kwa lolote lakini gesi kupelekwa Dar es Salaam.
Walioonekana jana kwa Rais Kikwete ni George
Mkuchika (Newala), Anna Abdallah (Viti Maalumu), Hawa Ghasia (Mtwara
Vijijini) na Agnes Hokororo (Viti Maalumu).
Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote iliyopatikana kuhusu uwapo wa wabunge hao Ikulu.
No comments:
Post a Comment