MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdenego Damian,
maarufu kama ‘Belle 9’ leo anatarajiwa kuzindua rasmi video na wimbo
wake ‘Listen’, uzinduzi unaotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Club
Bilicanas, uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, mkali huyo kutoka Morogoro
alisema amekuwa katika maandalizi kabambe ya uzinduzi huo na hasa
ikizingatiwa kuwa itakuwa shoo yake ya kwanza tangu kuanza kwa mwaka
2013.
Alisema kupitia onesho hilo mashabiki watarajie kupokea mambo makubwa
kutoka kwake ambayo yatawafanya kutojutia kutoa fedha zao kuhudhuria
ndani ya ukumbi huo.
Mbali na Listen aliyoaiachia mwishoni mwaka 2012, Belle 9 amepata
kutamba na singo kadhaa zilizoweza kushika chati kwenye vituo mbalimbali
zikiwemo Sumu ya Penzi, Masogange, wewe ni wangu, Amerudi na
nyinginezo.
Katika kunogesha usiku wa leo pia wasanii kadhaa wanatarajiwa
kusindikiza wakiwamo Kala Jeremiah, Nikki Mbishi, Amiri Milli, Ben Pol,
Mansu –Li, Young Killer na wengineo, ambapo kiingilio ni sh 6,000 kwa
kila mtu.
No comments:
Post a Comment