
MBUNIFU wa shindano la Manywele Kimwana wa Twanga, Maimatha wa Jesse anatazamiwa kuibuka na shindano jipya litakalojulikana kama Kigoli wa Manywele.
Maimatha amesema kuwa shindano hilo la Kigoli litawahusisha wasichana wenye vipaji kemkem ikiwemo kucheza ambapo alisema mipango inafanywa ili mshindi azawadiwe gari.
Amesema
kila kitu kimekaa mkao wa kula na mwishoni mwa mwezi wa 3 shindano
litaanza kunguruma na bendi itakayotumika ni Extra Bongo Wazee wa
Kizigo.
Hata
hivyo Maimatha alikataa kusema iwapo shindano la Kigoli ndio mwisho wa
Kimwana wa Twanga alilokuwa analienda kwa kushirikiana na Twanga Pepeta.
“Hivi
ni vitu viwili tofauti, sidhani kama kutatokea hitilafu yoyote ya
shindano moja kati haya mawili kulimeza shindano lingine,” alisema
No comments:
Post a Comment