MFALME
wa Rhymes, Afande Sele juzi usiku alikumbwa na masahibu makubwa pale
alipolazimika kuruka kwenye gari huku likiwa kwenye mwendo ili
kumkimbiza mwizi aliyekwapua simu yake.
Hiyo
ilitokea Tandika katika chimbo jipya la vibaka linalojulikana kama
Côte_d'I voire ambapo wakati Afande Sele akiwa ndani ya gari aki-chat
kupitia simu yake ya mkononi, ghafla kibaka akamkwapulia simu yake
kupitia dirisha lilokuwa wazi.
Kuona
hivyo Afande Sele aliyekuwa amekaa kiti cha mbele cha abiria, akaamua
kuruka kupitia dirishani wakati gari likiwa bado lipo kwenye mwendo.
Afande
Sele aliyetangaza nia ya kugombea Ubunge uchaguzi ujao, akakimbizana na
kibaka huyo hadi makaburini lakini akapigwa chenga ya mwili na kurudi
mikono mitupu.
Msanii
huyo akawaambia wenzake aliokuwa nao kwenye gari, King Sapeto na Dr
Levy kuwa simu yake ilikuwa na mambo yake mengi muhimu ndio maana
ilimlazimu kuchukua hatua ile.
Licha ya juhudi na ushirikiano waliopewa na maaskari
pamoja na wakazi wa eneo lile, simu haikupatatikana lakini angalau line
pamoja na memory card zilipatikana jambo lilipompa ahueni Afande Sele
kwa vile kumbukumbu zake muhimu zilikuwa kwenye line na memory card.
Via Saluti 5
No comments:
Post a Comment