Roma Mkatoliki |
MKALI wa hip hop nchini, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’, amesema
mashairi ya wimbo wake wa ‘2030,’ ni hisia zake binafsi hajamsema wala
kumtukana mtu.
Roma alisema jana kuwa baadhi ya wasanii wanaoimba hip hop wamekuwa
wakimtuhumu kwamba baadhi ya mashairi ya wimbo huo yanawahusu wao,
akisema ni maneno tu ambayo aliona akiyaunganisha yanaleta maana.
Alisema muziki ni kipaji chake na hawezi kumuimba msanii yeyote katika
wimbo wake na kuwalaumu wenye fikra hizo kwa kusema mtu makini hawezi
akasema maneno kama hayo.
“Kiukweli mtu anayefikiria hawezi akasema hayo maneno, hao ni baadhi
ya wasanii ambao hawapendi maendeleo ya wenzao na kutaka kuchafua jina
langu, naomba mashabiki wangu wawe makini katika hili,” alisema Roma.
Roma ni kati ya wasanii wanaofanya vizuri katika muziki huo na sasa
anatamba na kibao chake cha ‘2030’ mbali ya kuwa na kazi nyingi ambazo
zinafanya vizuri.
No comments:
Post a Comment