EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, February 18, 2013

Waumini wamuaga Papa

Maelfu ya watu wamekusanyika katika uwanja wa kanisa la mtakatifu Petro wakihudhuria tukio la mwisho la baba mtakatifu Benedict wa 16 la kuwaombea waumini hadharani,
 Papa Benedict wa 16 awaaga waumini,Vatican
Hiyo ni ibada ya mwisho ya baba mtakatifu ya mwisho ya hadhara ya siku ya Jumapili kabla ya kuachia kabisa nafasi hiyo ya kuliongoza kanisa katoliki duniani.
Kimsingi misa hiyo ya mchana ya jumapili huwavutia watu wachache ikiwa ni pamoja na watalii lakini mara hii wamejitokeza maelfu kwa maelfu ya waumini katika uwanja huo kumshuhudia kwa mara yao ya mwisho papa Benedict. Inasaidikiwa kwamba watu 150,000 wanahudhuria misa hiyo ya wazi katika uwanja wa mtakatifu Petro.

Waumini wa kanisa Katoliki 
Waumini wa kanisa Katoliki
Wamuaga
Baadhi ya watalii wamesikika kusema kwamba wamefika katika uwanja huo kumuaga na kumtakia mema na zaidi ya yote, mtalii kama Amy Champion aliyetokea Uingereza anasema inahitaji ujasiri kufanya kazi ya Papa na vile vile wakati unapoamua kuachia ngazi.
Kuanzia Jumapili Jioni baba mtakatifu hatoweza kuonekana tena mbele ya hadhara katika kipindi cha wiki nzima, ambacho kanisa mjini Vatican linaanza kipindi maalum cha maombi na tafakari. Jumapili hii uongozi wa mji wa Roma uliongeza usafiri wa mabasi na Treni za chini kwa chini ili kusaidia kukabiliana na msongamano wa watu waliokuwa wanamiminika kuelekea Vatican pamoja na kutowa usafiri wa bure wa mabasi madogo kwa ajili ya wakongwe na walemavu.
Kujiuzulu kwake
  Makadinali wakishauriana punde baada ya papa kujiuzulu tarehe 11 Februari 2013
Kiongozi wa kanisa Katoliki baba mtakatifu Benedict wa 16 aliushtuwa ulimwengu wiki iliyopita kwa kutangaza anajiuzulu kuanzia Februari 28, kitendo ambacho hakijawahi kushuhudiwa na kanisa hilo kwa kipindi cha miaka 600. Wakati Makadinali wakitazamiwa kumchagua mrithi wake mpya katika kikao maalum cha siri, baba mtakatifu Benedict mwenye umri wa miaka 85 atakuwa katika mapumziko na kufanya ibada katika makazi ya kanisa huko Kusini mashariki mwa mji wa Roma.
Baada ya wiki kadhaa anatazamiwa kuhamia kwenye makaazi mengine yaliyoko kwenye eneo la Vatican ambako ataishi maisha ya kitawa. Makao makuu ya kanisa hilo Katoliki mjini Vatican hayajatangaza tarehe ya kuanza kwa kiao cha siri cha kumchagua kiongozi mpya lakini yametangaza kwamba kikao hicho huenda kikafanyika mapema kabla ya mwezi March 15 na tarehe hiyo mpya inaweza kutangazwa chini sheria za sasa za kanisa.
Papa Benedikt XVI katika misa ya Jumatano ya majivu Februari 13,2013Papa Benedikt XVI katika misa ya Jumatano ya majivu Februari 13,2013
Uchaguzi wa papa mpya
Papa atahitajika kutia saini juu ya tarehe hiyo kitendo ambacho kitakamilisha kabisa kipindi chake cha takriban miaka 8 ya uongozi wa kanisa. Wakati huohuo tayari makadinali wameshaanza kuwasili Roma kuanza kipindi cha kujadiliana kwa mujibu wa sheria za kanisa kuamua ni kina nani walio wagombea wenye nafasi nzuri ya kuchukua wadhifa huo wa papa. Askofu mkuu Robert Sarah mzaliwa wa Guinea, ambaye ni kadinali anayeongoza ofisi ya misaada ya Vatican amewaambia waandishi wa habari kwamba viongozi wa kanisa watapaswa kumchagua papa mpya kwa utulivu na kuaminiana.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate