KOCHA Mkuu wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, Ernie
Brandts amesema mechi ijayo dhidi ya Azam FC, inamnyima usingizi
kutokana na kiwango na nafasi waliyonayo wapinzani hao kwenye mbio za
kuwania ubingwa.
KOCHA Mkuu wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, Ernie
Brandts akiwa nje ya uwanja katika picha juu.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Brandts alisema licha ya timu yake kuwa imara kwa sasa, anahofia mechi hiyo ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Brandts alisema licha ya timu yake kuwa imara kwa sasa, anahofia mechi hiyo ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
“Naamini uwezo wa timu yangu, ila hata wapinzani wetu ni wazuri. Ndiyo
maana naifikiria sana hiyo mechi japokuwa ni ya kawaida kama nyingine,
tatizo kubwa ni nafasi ambayo tunagombania nao, tunawazidi pointi tatu
tu,” alisema Brandts.
Brandts alisema mbali ya kuiwazia mechi hiyo, atapigana kufa na kupona
ili mwakani timu yake iweze kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kama
ilivyo Simba kwa mwaka huu.
“Naumia sana kuona timu yangu haishiriki katika michuano hii ambayo ni
moja ya nafasi ya kuwapeleka nje ya nchi wachezaji, najitahidi
nitakavyoweza mwakani lazima tushiriki na sisi,” alisema Brandts.
Naye Ofisa habari wa klabu hiyo, Baraka Kazuguto alisema kikosi chao
jana kilikuwa kwenye mapumziko, na leo kitaendelea na mazoezi kwenye
Uwanja wa Bora Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Yanga ndio vinara wa ligi hiyo kwa pointi 36; ikifuatiwa na Azam yenye
pointi 33, huku Simba ambao ni mabingwa watetezi, wakiwa nafasi ya tatu
kwa pointi 28.
No comments:
Post a Comment