WIMBO unaokwenda kwa jina la ‘Fulani’ ambao umeimbwa na mkali wa
muziki huo, Richard Shauri ‘Rich One’ umeanza kufanya vizuri katika
vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rich One
alisema, katika kazi hiyo ameshirikiana vema na wakali wa muziki huo,
Inspector Haroun na Juma Nature.
Rich One, aliwataka mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi
zake kama ilivyokuwa awali, ikiwa ni pamoja na video ya kazi hiyo.
“Namshukuru Mungu, kazi hii imepokewa vizuri na mashabiki, naamini
uwepo wa wakongwe niliowashirikisha, umenipa sapoti kubwa katika wimbo
huo,” alisema Rich One.
Alisema kwa sasa amejipanga kufanya vizuri katika soko na amerudi kivingine kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wake.
Msanii huyo alisema kazi hiyo aliifanya katika studio maarufu ya Halisi Records ya jijini la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment