Akizungumza
na mwandishi wa habari hii hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Aunt
alisema ndoa yake ina thamani kubwa na anatambua ndiyo maana yupo makini
kuilinda ili isivunjike kwa namna yoyote.
“Mimi natambua thamani ya
ndoa na namna ambavyo mwanamke anatakiwa kufanya kwa mume wake. Mimi
siyo aina ya wale wanaotamani kuvaa shela tu. Siyo mimi kabisa,” alisema
Aunt.
Hata hivyo alipotakiwa kuwataja baadhi ya mastaa ambao wameolewa kwa
lengo la kuvaa shela na si ndoa alikataa, akasema: “Wanajulikana vizuri
sana. Hata hivyo sipo kwa ajili ya kuwazungumzia watu wengine.
“Ninachosema mimi kama Aunt nitailinda ndoa yangu kwa nguvu zangu zote ili nisiabike. Unajua kila kitu kinafanyika kwa mapenzi. Ninajiamini nilimpenda mume wangu kabla na bado nampenda na nitampenda milele, hivyo lazima niwe mbunifu ili niwe wake wa milele.”

No comments:
Post a Comment