EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, March 13, 2013

MIMBA NI KIGEZO CHA KUOANA?

WAKATI wa kuongeza kitu ubongoni kuhusu uhusiano na mapenzi umewadia. Ni imani yangu kuwa kila wakati umekuwa ukijifunza mambo mbalimbali kupitia kona hii. Kama ni mara ya kwanza kujiunga nami fahamu kwamba huna cha kupoteza kwa kuwa memba wa All About Love. Karibuni sana.
 
Nakwenda kwenye mada; nazungumzia suala la mimba au ujauzito kwa maneno mengine. Hivi, hujawahi kusikia msichana akilazimishwa kuolewa kwa sababu amepata mimba? Je, hujawahi kusikia msichana aking’ang’aniza ndoa baada ya kuwa amepata mimba?
Bila shaka ni mambo ambayo umekutana nayo katika jamii inayokuzunguka. Kama halijawahi kukukuta moja kwa moja basi hata kwa ndugu, jamaa au rafiki zako. Hilo ndilo nililolipa nafasi ya kulijadili leo katika ukurasa huu.

KWA NINI TUNAJADILI?
Kwa bahati mbaya sana wengi wetu tumekuwa na tabia ya kujadili mambo ambayo tayari yameshakuwa matatizo. Hapa namaanisha kwamba, baada ya tatizo kutokea ndipo tunapotafuta ufumbuzi.
Mfano, wasichana wengi siku hizi huwa hawajali sana suala la matumizi ya kondom kwa sababu tu tayari ameshafahamiana na patna wake kwa muda wa miezi miwili mitatu – tayari wameshaaminiana!
 
Jambo hili siyo sawa kabisa na ndiyo maana leo tunajadili jambo hili. Unajua wanawake wakati wakikubali kukutana na wenzi wao bila kinga wala tahadhari yoyote huwa hawafikirii kabisa suala la kupata ujauzito lakini ikishatokea ndiyo wanatafuta utatuzi.
Ndugu zangu, kuna utatuzi gani hapo zaidi ya kuzaa? Hapo sasa ndipo linapoibuka suala la baadhi kukimbilia kutoa! Athari zake hapo ni nyingi na leo sitazingumzia kwanza.

UPO USHAHIDI
Tusiende mbali sana, ngoja nikupe ushuhuda huu; wasichana tisa kati ya 10 wanaonipigia simu kuomba ushauri, katika maelezo yao huwa wanaeleza wazi kuwa hawatumii kinga yoyote wala tahadhari ya kujihami na mimba.
Sababu nyingi zinazotolewa na wasichana hao ni kwamba wanaaminiana. Wengine huthibitisha kuwa wameshafanya hadi kipimo cha ukimwi hivyo hakuna shaka ya kutumia kinga. Ukiuliza kuhusu mimba, hubaki kujiumauma!
TAZAMA SASA...

Baada ya hayo yote niliyoeleza hapo juu, twende kwenye kiini chenyewe sasa. Hapa namzungumzia mwanamke ambaye tayari ameshapata ujauzito kabla ya ndoa. Ni mimba ya boyfriend tu. Hapa ndipo mahangaiko yanapoanzia.
Msichana anahaha, tena mbaya zaidi wazazi au walezi wake wanakuwa wameshatambua kuwa binti yao ni mjamzito. Swali la kwanza binti kuulizwa na wazazi wake litakuwa: “Hiyo mimba ni ya nani?”
Akimtaja tu baasi! Atapelekwa mkuku huko au atafukuzwa na kutakiwa aende kwa mwanaume wake au busara itatumika kuzikutanisha familia mbili lakini lengo likiwa moja, vijana hao waunganishwe.

NI SAHIHI?
Kwa hakika siyo sahihi hata kidogo. Kwa maamuzi ya haraka mzazi anaweza kuona njia nyepesi ya kumuondolea aibu nyumbani kwake ni kumuoza au kumpeleka binti yake kwa mwanaume aliyempa mimba lakini athari zake ni nyingi – tutaziona baadaye.
Suala la kuoana ni maridhiano ya ndani kabisa. Inawezekana vijana hao kwa kudanganyana kwao au kwa kutokuwa makini kumewafanya wajikute tayari wapo kwenye matatizo. Inawezekana kipaumbele cha uhusiano wao haikuwa ndoa.
 
Vijana wanapaswa kupewa muda wa kutafakari kwanza tatizo ambalo limejitokeza ambalo kwa hakika limetokea kwa uzembe wao wenyewe. Nasema uzembe kwa sababu kwanza hairuhusiwi watu walio nje ya ndoa kukutana kimwili.
Pili, pamoja na kukiuka utaratibu huo hawakuwa makini kujikinga na upatikanaji wa mimba hiyo. Hilo ni tatizo lao ambalo wanapaswa kujadiliana pamoja. Si ajabu uhusiano unaweza kuwa mzuri kwa binti kupata matunzo mazuri na baadaye kujifungua kisha taratibu nyingine (kwa hiyari yao) za ndoa zikafuata wote wakiwa na furaha na tendo hilo.
Si jambo zuri mwanamke kujipeleka kwa mwanaume kwa sababu tu amepata mimba. 

Vilevile si sahihi kumfukuza binti au kumlazimisha mwanaume aliyempa mimba aishi naye tena wakati mwingine bila ya ndoa kwa sababu tu amepata mimba.
Wiki ijayo nitakuwa hapa ambapo nitafafanua athari ambazo zinaweza kujitokeza ikiwa binti ataolewa/ataishi kilazima kwa mwanaume aliyempa ujauzito. Pia nitatoa ushauri kwa wanawake juu ya nini cha kufanya ili kujiweka salama katika hatari ya kupata mimba zisizotarajiwa.MADA NA JOSEPH SHALUA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate