NYOTA wa soka Carlos Tevez amekamatwa na polisi kwa kuendesha gari wakati akiwa amefungiwa.
Mshambuliaji huyo wa Manchester City, 28, anakabiliwa na adhabu ya kutumikia kifungo jela kama atashitakiwa na kutiwa hatiani.
Tevez
aliyefungiwa kuendesha gari kwa miezi sita, Januari mwaka huu
alikamatwa akiendesha karibu na nyumbani kwake, Alderley Edge, Cheshire,
Alhamisi jioni na akapelekwa kituo cha polisi cha Macclesfield.
Staa huyo baadae aliachiwa kwa dhamana.
Mahakama
ya Manchester ilimpiga marufuku staa huyo wa kimataifa wa Argentina
baada ya kukiri makosa ya kushindwa kutoa taarifa zinazohusiana na
kuendesha mwendo kasi uliovuka kiwango gari lake aina ya Hummer.
Tevez pia pia alikiri kutokuwa na leseni sahihi ya kuendesha gari Uingereza.
No comments:
Post a Comment