KAMA unaamini wachungaji wote watakwenda peponi basi utakuwa
unakosea. Hebu sikia hii. Mchungaji mmoja aliyejulikana kwa jina la
Michael Njoroge kutoka nchini Kenya amekumbwa na skendo nzito baada ya
mwanamke mmoja ambaye ni changudoa kuibuka hadharani na kudai
alinunuliwa na pastor huyo kwenda kanisani kutoa ushuhuda wa uongo,
Amani limeinyaka.
Kwa
mujibu wa mitandao mbalimbali ya nchini humo, kahaba huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Ester Mwende, awali alifuatwa na mtumishi
huyo wa Mungu na kumtaka wafanye mapenzi zoezi ambalo lilifanyika.
Akasema
baada ya zoezi hilo, ndipo mtumishi huyo wa Kanisa la Fire Ministries
Embakasi alimtaka afike kanisani hapo ili kutoa ushuhuda wa uongo na
kumuahidi kwamba angemlipa kiasi cha shilingi 10,000 za Kenya (kama 180,
000 za Tanzania).
Mwande ambaye alikuwa akitoa ushuhuda huo kwenye Kituo cha NTV cha nchini humo, alisema alikubali na kesho yake alikwenda kanisani kwa mchungaji huyo anayesifika sana kwa miujiza na upako.
Mwande ambaye alikuwa akitoa ushuhuda huo kwenye Kituo cha NTV cha nchini humo, alisema alikubali na kesho yake alikwenda kanisani kwa mchungaji huyo anayesifika sana kwa miujiza na upako.
Akasema: Nilipofika nilikaa na kujifanya nimepinda midomo. Muda wa
maombezi mchungaji akasimama na kusema mimi nina matatizo, nimepinda
midomo kwa sababu kuna kanisa nilikwenda nikasema kuna mchungaji amebaka
mtu kwa hiyo pigo langu lilikuwa kupinduka midomo.
Mwande aliendelea kusema kwamba mpaka anatoka kanisani hapo bado alikuwa amejipindisha midomo jambo lililomfanya kila mtu aliyemuona aamini.
Mwande aliendelea kusema kwamba mpaka anatoka kanisani hapo bado alikuwa amejipindisha midomo jambo lililomfanya kila mtu aliyemuona aamini.
Akasema kesho
yake alirudi tena na muda wa watu kushuhudia uponyaji, yeye alitoka
mbele. Mchungaji alipomwona aliwaangalia watu na kuwaambia: Huyu mama ni
yule aliyekuja jana akiwa amepinduka midomo kwa sababu ya kuwasema
vibaya watumishi wa Mungu.
Mwande alisema alishuhudia kwamba baada ya maombezi ya siku iliyopita anamshukuru Mungu alimponya na midomo yake iko sawasawa kama zamani, kauli iliyosababisha kanisa zima kulipuka kwa shangwe za kumtukuza Mungu.

Mwande alisema aliamua kuweka wazi madai hayo baada ya mtumishi huyo
kumrusha fedha nyingine walizokubaliana akidai kwamba mbali na yeye pia
mchungaji huyo alimtaka amtafutie makahaba wengine watatu, jambo ambalo
alilitekeleza lakini nao pia hakuwalipa.
Makahaba wenzake Mwande, wao walisema walimtumikia mtumishi huyo kwa kutoa shuhuda za uongo lakini hakuwalipa ujira wao na walipomfuata aliwajeruhi miguuni.
Makahaba wenzake Mwande, wao walisema walimtumikia mtumishi huyo kwa kutoa shuhuda za uongo lakini hakuwalipa ujira wao na walipomfuata aliwajeruhi miguuni.
Walisema baada ya tukio hilo, walitoa ripoti kwenye Kituo cha Polisi
cha Embakasi lakini maafande hao walikuwa wakisuasua kumtia mbaroni
mtumishi huyo.
CHANZO CHA HABARI GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment