Muungano cha CORD nchini Kenya umetaka zoezi la kuhisabu kura za uraisi
nchini humo lsitishwe na kuelezea wasiwasi wake juu ya uadilifu wa zoezi
ambalo siku tatu baada ya upigaji kura limeshindwa kukamilika.
Kauli hii inatajwa kwamba inaweza kuutia kasoro kubwa uchaguzi wa hapo
Jumatatu (tarehe 4 Machi), ambao hadi sasa umetajwa na waangalizi wa
kimataifa kwamba ulikuwa wa amani na wa wazi.
Mgombea wa CORD, Waziri Mkuu Raila Odinga, yuko nyuma ya mgombea wa muungano wa Jubilee, Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta, wakati kura zikiendelea kuhesabiwa.
Mgombea wa CORD, Waziri Mkuu Raila Odinga, yuko nyuma ya mgombea wa muungano wa Jubilee, Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta, wakati kura zikiendelea kuhesabiwa.
Hata hivyo, mgombea mwenza wa Odinga, Kalonzo Musyoka (pichani juu),
amesema kauli ya muungano huo haipasi kuchukuliwa kama wito wa umma
kuchukua hatua na amewataka wapiga kura kuendelea kuwa watulivu na
wastahmilivu.
Ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini humo, zilipelekea kiasi cha watu 1,200 kuuawa na zaidi ya 600,000 kulazimika kuyahama makaazi yao.
"Sisi kama muungano wa CORD tunaamini kwamba zoezi hili la kuhisabu kura limekosa uhalali na lazima lisimamishwe na liazishwe upya kwa kutumia fomu kutoka vituo vya kupiga kura," Musyoka aliwaambia waandishi wa habari.
"Tuna ushahidi kwamba matokeo tunayopokea 'yamechezewa,'" alisema.
Ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini humo, zilipelekea kiasi cha watu 1,200 kuuawa na zaidi ya 600,000 kulazimika kuyahama makaazi yao.
"Sisi kama muungano wa CORD tunaamini kwamba zoezi hili la kuhisabu kura limekosa uhalali na lazima lisimamishwe na liazishwe upya kwa kutumia fomu kutoka vituo vya kupiga kura," Musyoka aliwaambia waandishi wa habari.
Tume kuendelea kuhisabu kura
Viongozi wa muungano wa CORD, Raila Odinga (kushoto), Kalonzo Musyoka (katikati) na Moses Mutangula.
Hata hivyo, afisa mmoja wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka
(IEBC) ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba zoezi la kuhisabu
kura halitasitishwa.
Tume hiyo imekuwa ikisisitita kwamba zoezi zima limekwenda kwa haki na
uwazi na kwamba matokeo ya uchaguzi huo hayataathiriwa na kuharibika kwa
mitambo ya kieletroniki ya kuhesabia kura, ambayo imelifanya zoezi hilo
kwenda taratibu.
Kufikia sasa, Kenyatta anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kikabila
katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) anaongoza katika matokeo
hayo, huku karibuni nusu ya kura zikiwa zimeshahisabiwa.
Wafadhili kutoka nchi za Magharibi, wanaotoa msaada wa mamilioni ya dola
nchini Kenya kila mwaka, tayari wameonyesha kuwa kushinda kwa Kenyatta
kutaathiri uhusiano wa kidiplomasia.
Idadi ya kura zilizoharibika
Mwenyekiti wa IECB, Ahmed Issack Hassan (kushoto).
Mwenyekiti wa IEBC, Ahmed Issack Hassan, amesema kuhisabiwa
kwa kura huenda kukakamilika siku ya Ijumaa au Jumatatu, ambayo ni siku
ya mwisho kwa mujibu wa sheria, ambapo matokeo hayo yanapaswa
kutangazwa.
Pamoja na kufeli kwa mfumo wa kieletroniki wa kuhisabia kura, jambo
jengine linaloweza kuzua mzozo ni iwapo idadi kubwa ya kura
zilizokataliwa itahesabiwa katika matokeo ya jumla, maana hatua hiyo
inaweza kumzuia Kenyatta kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura ambazo
mgombea urais anapaswa kupata ili ashinde katika duru ya kwanza. Kwa
sasa tume ya uchaguzi inatangaza idadi ndogo ya kura zilizokataliwa
ukilinganisha na hapo awali.
“Nataka pia kusisitiza kuwa licha ya kuacha kutumia mfumo wa kuhesabu
kura wa elekroniki, haimaanishi kuwa uadilifu wa matokeo umeharibika,”
Mwenyekiti wa IEBC, Issack Hassan, amewaambia waandishi wa habari.
Wakenya wengi wanasema wameamua hawatakubali uchaguzi kusababisha mzozo
wa kikabila, baada ya uchaguzi uliopita kuathiri nchi hiyo yenye uchumi
mkubwa Afrika ya Mashariki.
No comments:
Post a Comment