Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa
urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka
raundi ya pili ya uchaguzi. Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema
Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo
kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada
yawakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu
na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.Waandishi wa BBC wanasema iwapo Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi ya mshindi baadaye leo
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment