WANAWAKE wametakiwa kujitokeza na kuondoa shaka juu ya mikopo
kwa sababu ni kwa ajili ya maendeleo yao na si kwa ajili ya
kuwakandamiza.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, alipokuwa akizungumza katika madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kawe Jijini Dar es Salaam.
Sadick alisema uwoga wa wanawake unawafanya wanashindwe kukopa kwa sababu ya kuhofia riba wanayotozwa.
Alisema wakati umefika kwa wanawake kuamdokana na fikra hizo kama wanataka kupiga hatua kubwa kiuchumi.
Mnatakiwa kuthubutu ili muone matunada yake na siyo kusiliza maneno ya mtu aliyeshindwa,îalisema sadick
Aidha aliwapongeza wanawake wajasiriamali kwa hatua yao nzuri ya kuweka vitambilisho vya bidhaa zao, hatua ambayo alisema ni maendeleo.
Aidha aliwapongeza wanawake wajasiriamali kwa hatua yao nzuri ya kuweka vitambilisho vya bidhaa zao, hatua ambayo alisema ni maendeleo.
ìNi hatua nzuri inayoonyesha mafanikio makubwa
kwa wananchi na tunaweza kufanya biashara sasa hata ya kimataifa
tukitambulika kama Tanzani,îalisema.
Aliongeza kuwa kutokana na hatua hiyo hata soko la Tanzani litakuwa kubwa na la kuaminika.
No comments:
Post a Comment