Irene Uwoya
MWANADADA
mwenye mvuto katika tasnia ya filamu Bongo Irene Uwoya amerudi tena kwa kuingia
na filamu ya Last Card msanii huyo alikuwa kimya kidogo kwa ajili ya maandalizi
ya filamu na sasa ameingia na last card kazi anayoaamini kuwa itafanya vizuri
katika soko la filamu kutokana na uzuri wa kazi hiyo kuandaliwa kwa umakini
zaidi,
Maneno
ya Uwoya“Ninafungua mwaka kwa bonge la filamu, sitaki kuwaambia kilichopo ndani
ya filamu ya Last card bali mtu akibahatika kuiona atasema mwenyewe kuwa kazi
hiyo kwa nini imeitwa Last Card, ni kazi bora sana kwangu na wote tulioshiriki
katika filamu na naweza kuwahakikishia wapenzi wa kazi zangu kuwa hii ni kiboko
si ya kuikosa,”anajitamba Irene.
Filamu
ya Last Card inakutanisha Irene Uwoya na mwigizaji mwenye sifa za filamu za
kimahaba nchini Baba Haji na kuifanya filamu kuwa na visa mikasa ya kuvutia
zaidi, inasemeka kuwa Baba Haji ndio msanii ndio msanii pekee bingwa wa kuigiza
filamu za mahaba Bongo mwenye uwezo wa kubembembeleza na kushawishi, pia
katika filamu hiyo unakutana na wakali wengine kama Janeth Sospeter, Omary
Barafu na wasanii wakali katika tasnia ya filamu Bongo, filamu hiyo inasambazwa
na Steps Entertainment.
No comments:
Post a Comment