MWIGIZAJI
Nyota katika tasnia ya filamu Wastara Juma ‘Stara’ amesema kuwa baada ya muda
mwingi wa mihangaiko ya kuuguza na hata kumpoteza mumewe anahitaji kupumzika na
kujenga akili upya, katika kulifanya hilo ameamua kwenda kupumzika Uarabuni kwa
ajili ya kutuliza akili na kujipanga upya
Wastara Juma ‘Stara’
“Nina safari kwenda Uarabuni kwa
ajili ya kupumzika kisha baadae kuangalia nafanyaje kazi katika staili ipi, kwa
sasa itakuwa ngumu kuwepo bila kufanya kazi lakini pia familia imeamua niende
huko kama ni sehemu ya kunifariji zaidi kutokana na kipindi hiki
kigumu,”anasema Stara.
Lakini mwanadada huyo asiye na makuu ameamua
kwenda huko kupmzika kutokana na hali ya filamu ilivyo sasa ambapo
watayarishaji wanajikuta wakikikaa kwa muda mrefu wakisotea kazi zao kutoka
pasipo na wakati maalum, soko la filamu kwa sasa inasemekana ni gumu kuliko
ambavyo jamii inaliona ukiona kazi imetoka sokoni ujue watu wametabika kwa
kiwango kikubwa.
No comments:
Post a Comment