Jeshi la Nigeria limesema limewaua wanamgambo 52 wa kundi la Boko Haram na kuwatia nguvuni wanachama 70 wa kundi hilo.
Wanamgambo wa Boko Haram wakiwa wamejizatiti kwa silaha
Msemaji wa Kikosi Maalumu cha Jeshi la Nigeria Luteni Kanali Sagri
Musa amesema wanamgambo hao wammeuawa katika mapigano ya siku 10 ambayo
yamekuwa yakiendelea katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi
hiyo. Ameongeza kuwa kati ya waliouawa ni makamanda 10 wa kundi hilo la
kigaidi ambalo limekuwa likitekeleza hujuma nchini Nigeria.
Msemaji huyo wa jeshi la Nigeria ameendelea kusema kuwa wanamgambo hao wamepokonya idadi kubwa ya silaha katika opareshini hiyo.
Tokea mwaka 2009 wanamgambo wa Boko Haram wametekeleza mauaji katika
maeneo kadhaa ya Nigeria. Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasana
malefu ya watu wameuawa katika hujuma za Boko Haram.
No comments:
Post a Comment