Habari na saluti5-Tanzania
MWANAFUNZI wa kiume mwenye umri wa miaka minane amemuoa mama mwenye umri wa miaka 61.
Kijana
huyo Sanele Masilela alisimama mbele ya watu 100 na kufunga ndoa na Bi
Shabangu, mama mwenye watoto watano ambaye tayari ni mke wa mtu.
Wawili
hao walivalishana pete na kupeana mabusu motomoto Katika sherehe
zilizofanyika Tshwane nchini Afrika Kusini, huku Sanele akidai mizimu ya
mababu zake walimuamuru afunge ndoa hiyo.
Hata hivyo ‘wana ndoa’ hao hawakusaini cheti cha ndoa na wala hawaishi pamoja.
Selele
alisema: “Nilimwambia mama yangu kuwa nataka kuoa, nina furaha kumuoa
Hellen, nitakapokuwa mkubwa nitamuoa mwanamke wa rika langu”.
Mama
wa Selele mwenye umri wa miaka 46 alisema babu wa mwanae alimtaka
mjukuu wake aoe kabla hajafariki na akamchagua Hellen kwa kuwa
alimpenda.
“Kwa kufanya hivyo mizimu ilifurahi. Kama asingetii basi jambo baya lingetokea kwenye familia.
No comments:
Post a Comment